Mshambulizi
wa Manchester City Mario Balotelli amezozana na kocha wake Roberto Mancini
wakati walipokuwa mazoezini.
Picha za
wawili hao wakivutana mashati zimesambazwa kwa vyombo vya habari na inasemekana
zilizchukuliwa mapema hii leo wakati walipokuwa mazoezini katika uwanja wa
Carrington.Picha hizo zimeonyesha wachezaji wengine na maafisa wa klabu hiyo
wakijaribu kuwatenganisha.
Hata hivyo
klabu hiyo imekataa kuthibitisha au kukanusha madai hayo.Mancini anatarajiwa
kujibu maswali kuhusu tukio hilo wakati atakapofanya kikao na waandishi wa
habari siku ya Ijumaa.
No comments:
Post a Comment