Friday, January 4, 2013

Fahamu madhara ya kuongeza makalio



VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini) baada ya muda mfupi.



Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya binadamu.
Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika mpangilio usio sahihi.
Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa  saratani.
Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu".
Anaongeza: "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi. Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa." alisikika akisema.
Mpaka kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu 278,000 wanaotembelea huku ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000 wakipeleka katika kurasa zao.
Mtumiaji mmoja wa mtandao huo kutoka nchini Marekani Donna Wright-Levy, alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda maeneo kadhaa ambako hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina ulazima wa kwenda kupima saratani".
Ni vigumu kuthibitisha mwanamke huyu alitumia kliniki gani wakati alipofanyiwa uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake miaka miwili iliyopita.
Lakini mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya upasuaji ya BAAPS Aurora nchini Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni mshauri wa upasuaji anaamini kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho ya makalio yake kwa dawa za silicone.
Alisema tatizo hutokea wakati nyama ya makalio inaposhindwa kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa na hivyo madhara huanza kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya nyama na baadaye mfupa.
Ni matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji ya dawa za kuongeza ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni lazima itokee baada ya muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina maana wakati wake ukiisha kitarudi kama awali.
"Huyu mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma na kwa juu zaidi hivyo tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana hakufanya upasuaji bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema Richards.

No comments:

Post a Comment