Thursday, May 30, 2013

BADO NI MAJONZI JUU YA KIFO CHA ALBERT MANGWEA


Kenneth Mangwea kaka wa marehemu Albert Mangwea ana neno kwako.
Kenneth jana alikua na majozi kwa kila kinachoendelea kuhusiana na msiba wa mdogo wake! kwamba msiba huo usichanganywe na siasa ama suala lingine lolote, zaidi anachoomba ni ushirikiano, na ushiriki wa namna yoyote ili kufanikisha mazishi na maziko  ya mdogo wake.
BonnVencha Kilosa, producer wa kwanza kufanya kazi na Albert, na alifika pahala pa kumhoji Mann kwa tetesi za utumizi wa dawa za kulevya, hakupata jibu, akaweka watu wamchunguze alipokwenda London wapi hawakuona kitu, anashangazwa na tetesi zinazoendelea kuvuma juu ya marehemu, Vencha amewataka wasanii kila mmoja kwa wakati wake kusimama imara kwenye game na kukamua kisawasawa, kama ipo ipo tu.
Taikuni Ally a.k.a Mchizi Moxie, huyu ni rafiki mkubwa wa Marehemu Albert Mangwea, wamekua pamoja mtaa mmoja wa Kijitonyama maeneo ya Makumbusho, Albert akiwa msanii chipkizi, wakasafiri pamoja safari ziso idadi kwa humu ndani ya Tanzania, lakini za nje ya mipaka anakumbuka Mombasa, Malindi na Uganda. alipopokea kifo cha mshkaji wake hakuamini na akaomba kuongea na walioko South Africa ili kuwaomba wamuashe sana mshkaji wake hajafa, kwani yeye anamfahamu sana rafikiye, akilala hulala kweli, lakini safari hii haikua sawa, Albert Mangwea amelala milele.

Mangwea na Mchizi Moxie walishirikiana katika kazi ya Mikasi(mann) na Demu wangu(Moxie), ambazo zili hit kinyama!.
Siku ya Vencha iliharibika vibaya mno, hali ilikua si hali.
Vencha na Kenny, wakibadlishana mawili matatu juu ya taratibu za mazishi ya Albert.
note
tunasubiri kusikia taarifa ya uchunguzi wa madaktari juu ya nini chanzo cha kifo cha msanii  Albert Mangwea , uchunguzi unafanywa  leo.

No comments:

Post a Comment