Baadhi ya vyakula
Umoja wa Mataifa umeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za
Tanzania kukabiliana na tatizo la lishe bora hasa wakati huu ambapo dunia
inapiga mwendo kuelekea kwenye malengo ya maendeleo ya mellenia. George Njogopa
na taarifa zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kitaifa
yenye lengo la kuboresha hali ya lishe Mwakilishi wa shirika la Umoja wa
Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Bwana Paul Edward alisema kuwa, Tanzania
imeendelea kupiga hatua kukabiliana matatizo yanayotokana na ukosefu wa lishe,
lakini hata hivyo bado kuna safari ndefu.
Kumekuwa na idadi kubwa ya vifo vya kina mama wanaojiandaa
kujifungua na vile vya watoto waliochini ya umri wa miaka hiyo mitano kutokana
na kile kinachoelezwa kwamba ni ukosefu wa lishe bora.
Rais Jakaya Kikweye aliyezindua kampeni hiyo amesema kuwa
serikali yake imedhamiria kukabiliana na tatizo hilo la lishe bora kwa
kuanzisha miradi mbalimbali.
Kampeni hii pia imelenga kupunguza kiwango cha watoto
wanaandamwa na matatizo ya kudumaa ambao wanafiia asilimia 40 kwa sasa.
No comments:
Post a Comment