Wednesday, May 29, 2013

R.I.P ALBERT MANGWEA




                                           Albert  Mangwea


Ni vigumu kuamini lakini taarifa ambazo tayari zimethibitishwa  kwamba Rapper, Freestyler, Albert  Mangwea amefariki dunia majira ya saa 9 alasili jana.

Inatajwa kuwa   baada ya kulala Albert hakuamka tena licha ya  Marafiki za Albert  kujaribu kwa kila hali kumuamsha Albert  lakini wapi hakuamka.na kifo chake kiligundulika  mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa.
 
Kwa mujibu wa Taarifa zilizotufikia usiku  wa jana inataarifiwa  kuwa mmoja kati ya marafiki zake ambao walikuwa pamoja karibu naye nchini humo msanii wa Bongo flavour aitwaye M2 Tha P naye anatajwa kuwa yuko hoi katika hospitali ya St Hellen akipatiwa matibabu kurejea katika hali ya kawaida.
 
Sababu za kifo cha Ngwea bado hazijatajwa na bado hakijajulikana kitu  kilichowasibu hata kutokea matukio hayo mfululizo.... Endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi.

FA, PINA WAAHIRISHA SHOW ZAO.
Wakati huo huo msanii Mwana FA ameahirisha show yake iliyokuwa ifanyike ijumaa hii jijini Dar es salaam, sambamba na msanii huyo Kala Pina Naye amesikika kupitia Amlpifaya akitanabaisha kuahirisha show yake hadi pale itakapo tangazwa tena rasmi.



Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment