Monday, May 27, 2013

WALIOKO PEMBEZONI NA MADHILA YAO


Kila familia huko Shinyanga vijijini kila aliyemo ni lazima ajifunze na kujua kutumia baiskeli, kama hujui basi utatembea umbali mrefu mno!

Haya ni maji ya kunywa kwa wenyeji wa shinyanga vijijini, ng'ombe,mbuzi,kondoo na hata punda wanakunywa maji kwenye lambo moja huku yakichanganyika na kinyesi na mkojo wa wanyama hao.
Magugu yakiwa ndani ya maji na maji hayo yalikua na vilui lui vinhiiii
Jirani kabisa na Lambo kuna kinyesi kinachotimbwa na ng'ombe na maji yanpotiririka hapo yanrudi lamboni na wenyeji huwa hawachemshi maji  ya kunywa bali  ya kunawa huchemshwa!
Huu ni uharo wa ng'ombe, ambapo ng'ombe akipita hapo anaingiza lamboni maisha yanaendelea.
Ng'ombe wakinywa maji hayo.
dada naye akiwa amesha chota maji ya lamboni tayari kwa matumizi yote ya nyumbani.

Niliwafumania wakinywa maji hayo ya lamboni papo hapo, bila ya kujali chochote, watafanya nini! ndo maisha,
FUATILIA JICHO LA TATU KUPITIA CLOUDS TV  ILI KUJUA NI KIJIJI GANI SHINYANGA VIJIJINI CHENYE HALI HII.

No comments:

Post a Comment