Kisa cha hivi karibuni cha Muasi nchini Syria kuula moyo wa
mwanajeshi aliyeuawa, kiliwashangaza wengi. Lakini tukio kama hili je ndilo la
kinyama zaidi kuliko matukio mengi yanayoshuhudiwa katika maeneo ya vita?
Tumezoea kusikia ripoti za makaburi ya halaiki, vyumba vya
mateso, mauaji na kukatwa katwa miili ya watu na hata kuwaangamiza watu katika
kijiji kizima.Lakini kitendo hiki cha kula moyo wa adui, bila shaka kimezua
hisia kali. Binadamu kumla mwenziwe ni jambo linalokiuka maadili na hata baadhi
ya imani za watu kuhusu kinachoweza kutendeka katika katika maeneo ya vita.
Kwa hivyo je ghasia za Syria zimefika kiwango gani na je ni
dalili gani za kuonyesha ikiwango hicho?Je ni nini kinachosababisha watu katika
maeneo ya vita kufika kiwango hiki cha kula wengine?Katika mahojiano na
wapiganaji 2,500 wa zamani kutoka Uganda, Rwanda, Colombia na Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo,
iligunduliwa kuwa vitendo vinavyofanyika katika maeneo hayo
sio vichache ukilinganisha na kile kichotokea nchini Syria.Kinyume na hilo,
wakati maadili ya kijamii yanapoporomoka huku ghasia zikianza kutokea ishara ya
vita, basi maadili yanayolinda binadamu kutokana na binadamu mwenzake nayo
yanapotoka.
Kumuona mwathiriwa akiteseka humridhisha mshambuluaji na
kuliona jambo hilo kama zawadi au tuzo kwake.Kuna sababu mbili zinazomsababisha
mtu kufanya kitendo mfano kama cha kumla mwenziwe.Takriban watoto milioni mbili
wanakumbwa na utapia mlo nchini Syria
Kwanza , huwa kuna ghasia, ambazo hutokana na hisia za chuki
na hasira na hilo huonekana kama jibu kwa tisho lolote.Na pili kuna hisia za
kufurahisha, kuchangamsha na za raha tupu.Hakuna anayejua sababu ya kutokea
kitendo cha Syria na pili hakuna anayejua kilichomshinikiza yule muasi kufanya
kitendo kile.
Kitendo hiki hakiwezi kukubalika, lakini kinaweza kueleweka
ikizingatiwa matukio ya Syria (vita) ambavyo vimesababisha kutendwa kwa kitendo
kile.Kilitokana na hasira na hamu ya kulipiza kisasi. Binadamu wanaweza kufanya
vitu ambavyo vinaonekana kwenda kinyume na ubinadamu.
Kunyongwa kwa Saddam Hussein au mauaji ya Bin Laden
vinatukumbusha kuwa wakati mmoja binadamu wanaweza kukiuka maadili yao na kuua.Kanda
inayoonyesha kitendo cha mauaji na picha ya damu ya mtu kwenye chumba chake
huonekana kama tuzo baada ya uwindaji.Kitendo hicho pia ni kumbusho la mapigano
yanavyokithiri nchini Syria.
Mateso bila shaka huwa ni machungu kwa adui , ukataji wa
viungo vya mwili mfano maskio , midomo na sehemu za siri ni vitendo vya kawaida
katika vita na viko wazi katika maeneo mengi ya dunia.Na kwa hivyo kitendo
kilichoripotiwa Syria hakipaswi kuwashangaza wengi.Hali inaendelea kuzorota
nchini Syria ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ukiwa jambo la kawaidaNadhani
muhimu hapa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika Syria ambao ni
siri kubwa.Takriban watoto milioni mbili wanakumbwa na jnaa, magonjwa na
wameathirika kisaikolojia.
Kando na hilo,kuna makundi ya waasi ambayo huamua kula
binadamu kama njia moja ya kuendeleza uasi wao.Takriban asilimia 10 ya waasi
katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, walisema wamewahi kula binadamu na
kwamba waliwahi kushuhudia wenzao wakila binadamu.
Wapiganaji wa Mai-Mai, nchini DRC , walikuwa na tabia ya
kunywa damu ya adui wao na kula moyo au sehemu zao za siri wakiamini kuwa
viungo hivyo viliwapa nguvu dhidi ya maadui wao. Hata hivyo hakuna ushahidi
wowote wa kuwahi kutokea tabia ya watu kukulana Syria.Hata hivyo kuna uwezekano
kuwa kinachosahuhudiwa kwenye kanda hiyo ya video nchini Syria, ni kitendo
ambacho kitakuwa kitu cha kawaida nchini Syria.
hapa zatajwa sababu za askari huyo kuula moyo.
No comments:
Post a Comment