Wednesday, May 22, 2013

PICHA NILIZO CHAGUA KWA SIKU YA LEO


Kiukweli nawasifu sana wanaoyatengeneza matunda katika maumbo mbali mbali na mara kadhaa huwa natamani nami nijue namna ya kuyabuni maumbo mbali mbali kwenda katika matunda! msaada tafadhali, kwa ajuaye  anifundishe tafadhali.

napenda sana kuogelea , lakini nayaogopa maji! baada ya siku moja  kunitenda! nataka bado kurudi kwenye maji kwani nasikia ni dawa kubwa kwa ajili ya kupunguza mwili! but kwa picha hii ya leo nimependa mtoto huyu aliyeamua kujitupia majini na suti yake ya kuzaliwa ki style.
Ulaji kama huu, huwapunja watoto, lakini mi hupenda sana kula kwa mtindo huu, kwani hujenga umoja na mshikamano,na asiye na speed ya kula atakula tu! kushiba ni speed yako, hapo no mbwembwe wala kujivuta wakati wa kula, watoto wetu leo kula ni wavivuuu, baada ya kumuwekea kila mtu na sahani yae.
Natamani kujua ni mzuka gani ambao huwapata wanawake wenzangu na wasichana kiasi cha kuamua kuchukua viti na kujiweka katika mikao hii ya faragha! na watu hushangilia na kuwatunza! utamaduni wetu uknaelekea wapi? TAFAKARI!
ONE LOVE! nimeipenda sana hii picha mpaka na i feel, the way mtoto alivyoshika kidole gumba cha babake kiukweli hizi ndizo picha za siku ya leo nlizofanikiwa kuzipata.

No comments:

Post a Comment