Monday, May 27, 2013

HII NI WIKI YA HIP HOP MJENGONIII,TWAANGALIA FURSA,UTAMADUNI WA HIP HOP


Hamisi Mwinyijuma a.k.a mwana Fa, ama waeza mwita binamu! mwanamuziki mwenye elimu dunia na muziki anaumudu! na leo hii ni siku yake mjengoni katika wiki ya hip hop kabla ya kwenda kufanya kweli, get ready twenzetu!

Ancor wa power breakfast Babra Hassan akitabasamu na ku show Love kwa kua karibu na cousin!
Mwana dashosti huyu alishirikishwa na Binamu katika wimbo wa Unanitega? sikiza tena upime kipaji chake.

Gerald Hando akizungumza na mwana fa ambaye hayuko pichani.nyuma yake ni Paul James a.k.a Pj
 Paul James a.k.a Nyani Mzeiya akijiandaa na magazeti tayari kwa kuperuuzi na kudadis

Gerald akizungumza jambo huku Binamu akisikiliza kwa makini.

Wakati binamu akifuatilia simu yake, Babra Hassan akifanya kajiutundu! utangazaji wa redio raha, unajiachiiia! fanya hivyo tv uone jamii itakavyo nyanyuka na wewe kwi kwi kwi kwi.

Binamu akijibu swali la Gerald kwa umakini mkubwa.

Nyani mzeiya,ambaye ni Brand Manager wa Power Breakfast! namkubali sana mybrother.

Ah mzaramo Mbwiga, nimeshindwa kujua jina lake kamili oooooooh am so sorry! amevunja nne, hatareeee, anakuja juu kwa kasi ya ajabu! napenda mambo  yake kiukweli!

Chezeiya Nyani mzeiya weye! ametupiamo swaggar!!!!!!



katika historia ya muziki wa hip hop tanzania, kwa mara ya kwanza kabisa, mwana fa amekuandalia show ya kipekee itayokupa experience ya tofauti kabisa na shows zote ulizowahi kuzishuhudia, iite the finest. ni show maalum kwa ajili ya watu maalum ambayo itafanyika ijumaa hii ya tarehe 31 ndani ukumbi nadhifu wa makumbusho ya taifa opposite na chuo cha ifm….
mwana fa akiwa pamoja na the kilimanjaro band “wananjenje” watasindikizwa na ben pol, linah, mandojo na domokaya na ay…kama unataka kuingia kwenye list ya watu hawa maalum, basi nunua tiketi yako mapema kwa shilingi 50,000 tu…show nzima itaanza saa 3 za usiku….. experience the difference…experience “the finest”.

No comments:

Post a Comment