Angelina Jolie
Mcheza filamu mashuhuri duniani,Angelina
Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa
uzazi.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na
mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya
matiti.
Kulingana na Jolie madaktari
walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku
akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
Fikiria unapoteza viungo vyako ili kujiokoa.
Angelina akiwa na mamake alokua akiitwa
Marcheline enzi za uhai wake
Bi Jolie alieleza kuwa mamake
alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.
Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku
moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa
upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Brad Pitt,na Angelina Jolie, ameahidi kufunga ndoa mapema na mpenziwe japokua taarifa za ugonjwa wake zimezagaa.
Uwezekano wake wa kuugua saratani
sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa
kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na
kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu
kufanyiwa upasuaji.
No comments:
Post a Comment