Mwili wa marehemu
Anthery Mushi umezikwa kijijini kwao Ongoma bila huduma ya kikanisa. Familia
ililimuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo ili aridhie familia ya Anthery
isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.
Kanisa Katoliki,
Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo
chake.Watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha
ibada kutokana na taratibu za kanisa za kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya
Anthery.
Mtoto wa marehemu Alvin Anthery (ambaye alizaa
na Ufoo), hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.
Hata hivyo, hali
ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti
na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana,
ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery.
Kiongozi aliyeteuliwa
na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema
kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa
kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu
kubadilika na kuwa tembo: “Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya
kilichotokea maana mtbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana
na habari zinazotangazwa.
Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini
Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa
kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.
Anthery Mushi (40) alijipiga
risasi baada ya kumuua mkwewe, Anastazia Saro, na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo
Saro, (mtanzangaji wa kituo cha televisheni cha ITV), huko nyumbani kwao,
Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment