Monday, October 28, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA HIFADHI YA MAZINGIRA WA VIKUNDI VIDOGO VYA UCHAKATAJI MAWESE IGALULA MKOA WA KIGOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kuhusu maandalizi ya jinsi ya kukamua mafuta ya Mawese kutoka kwa Meneja wa mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Tanganyika, Seleboni John Mushi, wakati Makamu alipozindua mradi huo jana Igalula, Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal, alitembelea na kukagua mradi huo unaosimamiwa na Ofisi yake na kujionea jinsi mafuta hayo yanavyopatikana.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Vikundi vidogo vya Uchakataji Mawese Igalula Mkoa wa Kigoma, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Wilayani Uvinza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula. Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukamuaji wa mafuta ya Mawese Kaimu Meneja wa kutoka kwa Meneja Sido Mkoa wa Kigoma, Gervas Ntahamba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana Igalula, Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal, alitembelea na kukagua mradi huo unaosimamiwa na Ofisi yake na kujionea jinsi mafuta hayo yanavyopatikana.

No comments:

Post a Comment