Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs. Monica Mwamunyange
akisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano wa 7 wa
mapitio ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi kabla ya kufunga jana jioni. Kushoto
kwa NAibu Katibu Mkuu ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhitbi wa Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Bw. David Mziray.
Bw. Hassan Malik kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRL),
akiwasilisha mada ya utendaji wa Shirika hilo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika kwenye mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Uchukuzi jana jioni. Mkutano huo
wa siku mbili umewakutanisha wadau mbalimbali pamoja na wahisani kujadili
changamoto na nama ya kukabiliana na chngamoto zilizopo kwenye sekta ya
Uchukuzi.
Mwenyekiti wa washirika wa maendeleo, Dk. Yazuru Ozeki, akitoa hotuba
yake kwa niaba ya washirika wa maendeleo walioshiriki kwenye mkutano wa 7 wa
mapitio ya Sekta ya Uchukuzi,uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs. Monica Mwamunyange
akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya
Uchukuzi uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili. Hotuba hiyo ilisomwa
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment