Duniani kuna maajabu
mengi,kati ya maajabu hayo ni huu mgahawa uitwao Rock uliopo visiwani Zanzibar
uliojengwa juu ya mwamba mkubwa katika bahari ya Hindi.
Mgahawa huo
ulifunguliwa rasmi mwaka jana na kuna viti 45 ambapo wateja huchukuliwa na boti
maalum kutoka pwani hadi kupata huduma katika mgahawa huo ili wasikanyage maji
wakati wakiingia kwenye mgahawa huo.
Chakula kinachopatikana
muda wote katika mgahawa huo ni samaki pekee kutoka baharini na vinywaji.
Wafanyakazi wa The Rock
The Rock umetajwa kuwa
ni mgahawa wa ajabu katika Afrika Mashariki na watu wengi wakiwemo watalii
hupenda kwenda kutokana na habari zake kuenea kwa kasi na wengi hupendelea
kupata hewa safi ya baharini na kuona jinsi kilivyokuwa ndani.
Rock, ambayo
ilifunguliwa mwaka jana, inaweza kufikiwa kwa miguu, lakini pia kuna usafiri wa
mashua wa kuwasafirisha wateja kutoka pwani hadi kwenye mgahawa huo.
No comments:
Post a Comment