Wednesday, October 23, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00260
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]

 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 10. 2013.
WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA  ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
MNAMO TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA  SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA  MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI WALIMKAMATA SAMWEL S/O VITALIS @ MANDE , MIAKA 34, MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA  AKIWA NA SARE PAIR MOJA “KOMBATI”  ZA ASKARI WA WANYAMAPORI PAMOJA NA PINGU MOJA. MBINU NI KUTUMIA VIFAA HIVYO KATIKA UWINDAJI HARAMU.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI MALI ZA SERIKALI  ISIVYO HALALI KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU AU KIKUNDI KINACHOMILIKI MALI ZA SERIKALI /WAWINDAJI HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI  WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA  MBEYA MJINI  – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO].
MNAMO TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MANGA – MWANJELWA , KATA YA  MANGA , TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  WALIWAKAMATA 1. ITIKA D/O KIMANGA,, MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MWANJELWA 2. YASIWA S/O SHELISHELI, MIAKA 37, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA, 3. MATESO S/O SHELISHELI, MIAKA 33, MNYIHA,MKULIMA, MKAZI WA CHUNYA NA 4. EMANUEL S/O SILAVWE, MIAKA 33, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA  WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NANE [08]. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
WILAYA YA  MOMBA  – KUPATIKANA NA BHANGI. 
MNAMO TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA  SAA 05:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MJINI , KATA YA  TUNDUMA  , TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  WALIMKAMATA 1. EDMUND S/O KANFWA,, MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MWANJELWA NA  2. TAIFA S/O MWAMAHONJE, MIAKA 22, MMALILA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA MIGOMBANI – TUNDUMA WAKIWA NA BHANGI KETE 18 SAWA NA UZITO WA GRAM 90. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WAVUTAJI WA  BHANGI.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment