Washiriki wa mkutano wa 7 wa Mapitio ya Utendaji wa sekta ya
Uchukuzi, wakijitambulisha kabla ya mkutano huo wa siku mbili kuanza katika
ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jubilee. Mkutano huo wa 7 unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta
ya Uchukuzi kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta na kuzitafutia
ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Alhaj Mussa Iyombe, akitoa
hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa Sekta
ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la Golden
Jubilee.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na
Tathimini wa Wizara ya Uchukuzi , Bw. Aunyisa Meena, akiwasilisha mada kwenye
mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi, unaofanyika Tarehe
28-29 Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Golden Jubilee. Mkutano huo utajadili
maswala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison
Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya
utendaji wa sekta ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano uliopo
kwenye Jengo la Golden Jubilee(PSPF BUILIDNG). Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha
wadau wa taasisi mbalimbali za sekta ya uchukuzi kujadili njia mbalimbali za
kuboresha sekta ya Uchukuzi
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kushoto waliokaa), akiwa
katika picha ya pamoja na Mabalozi, wahisani wa Miradi ya Maendeleo na wajumbe
mbalimbali waliohudhuria mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya
Uchukuzi, Unaofanyika tarehe 28-29 Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la
Golden Jubilee. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Mrs. Monica Mwamunyange, kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
No comments:
Post a Comment