Monday, October 21, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


DSC00260

[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


 “PRESS RELEASE” TAREHE   20. 10. 2013. 
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUMGOGA MTEMBEA KWA    
                                                    MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
.
MNAMO TAREHE 19.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO KIJIJI CHA GARIJEMBE, KATA YA TEMBELE, TARAFA YA TEMBELE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA MBEYA. GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA WALA DEREVA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU {MTOTO} AITWAYE LUSI D/O SAFARI, MIAKA 12, MSAFWA, MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA SHULE YA MSINGI GARIJEMBE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALINI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA KYELA – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
                                    KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 19.10.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KIJIJI CHA MPUNGUTI, KATA KATUMBA – SONGWE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. GARI NO T.318 BYH AINA YA  CANTER LIKIENDESHWA NA DEREVA HAMZA S/O MSHANO, MIAKA 35, MMAKONDE,  LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE JULIUS S/O MWAMBELO, MIAKA 38, MNYAKYUSA, NA MKAZI WA ITENYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU BAADA YA UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUFANYA FUJO UWANJA WA MPIRA.
MNAMO TAREHE 19.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA UWANJA WA SOKOINE JIJI NA MKOA WA MBEYA. DAVID S/O CHARLES, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO KATIKA UWANJA WA MPIRA WA SOKOINE KWA KUWARUSHIA JIWE WACHEZAJI WA TIMU YA MPIRA WA JKT RUVU KATIKA MECHI DHIDI YA MBEYA CITY MARA BAADA YA MPIRA KUISHA KITENDO AMBACHO SIO TU KUWA NI UVUNJIFU WA SHERIA BALI PIA NI AIBU KWA WANA MBEYA NA WADAU WA MICHEZO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWE ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MASHABIKI NA WADAU WA MPIRA KUACHA VITENDO VYA FUJO NA VURUGU WAKATI WA MECHI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE ATAKAYEONA MTU/WATU WAKIFANYA FUJO BADALA YA KUFURAHIA/KUFUATILIA BURUDANI HUSUSANI KWENYE MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA ZINAZOENDELEA ATOE TAARIFA MARA MOJA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE .
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment