NAMNUKUU DADA YANGU
Betty Mkwasa
Baba Bhoke au ancle J
leo huzuni niliyonayo imenikumbusha akina Salama Mfamao, Siwatu Luwanda, Idd
Mchata, Omary Jongo, Hassan Mkumba, Tumbo Risasi, Nadhir Mayoka, Michael Katembo,
Henrick Libuda, Karim Besta, hao ni baadhi tuu, wakati wa uhai wao Radio
Tanzania wakati huo ikipasua mawimbi.
Nilianza kazi RTD ya kutayarisha muziki
ukiwa Boss wangu, na ulinifundisha kutayarisha kipindi cha Misakato na club
raha leo show tukiwa na marehemu Libuda, mpaka nilipoanza kusoma habari.
Hatimae tulikuja kuwa pamoja tena Radio one & ITV ukanipokea wewe, Ahmed
Kipozi na Charles Hilary.
Hapa duniani sote twapita!! Umetangulia Nyaisanga
ambaye Kwa utani wako mwingi Laura George ulimpachika jina la Hilary Clinton
huku mm ukinipachika jina la Monica lewinsiky, nasi tukakuita kibabu smoker!!
Sintasahau tulivyotaniana sana baada ya kumaliza kusoma habari tukiwa zamu pale
ITV. RIP Julius Mungu ailaze Roho yako mahala pema peponi AMINA!
No comments:
Post a Comment