Makamu wa Rais, Dkt. Mhammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi katika Hafla ya Chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M, maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa Kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 25, kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya NBC, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo ina lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya Kusomesha Kinamama wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto, ambapo jumla ya Sh. milioni 719 zilipatikana wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Chakula cha Hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Katika hafla hiyo jumla ya Sh. milioni 719, zilipatikana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwanafunzi Mkunga kutoka kabila la Kimasai, Toinoi Kayu Moringe (20) anayeendelea kupata elimu ya Ukunga katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Muheza cha St. Augustino, baada ya kutoa ushuhuda kuhusu elimu yake na mtazamo wa kabila lake kuhusiana na suala zima la elimu hususan kwa mtoto wa kike, wakati wa hafla ya chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage na Bank M, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, ijumaa usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea picha ya mchoro yenye thamani ya Sh. milioni 2.2 kutoka kwa wawakilishi wa NSSF walioinunua picha hiyo wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage na Bank M, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, ijumaa usiku.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda, akizungumza na kutoa shukrani kwa Wadhamini na wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla hiyo ya Usiku wa Chakula cha Hisani iliofanyika Jana usiku katika Hotel Ya Serena.
No comments:
Post a Comment