JULIUS NYAISANGA
MOROGORO
.. MTANGAZAJI na mwandishi wa habari wa siku nyingi JULIUS NYAISANGA maarufu kwa jina la uncle J amefariki dunia mkoani Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa kisukari na shinikizo la damu
Meneja wa matangazo kituo cha Abood Media ambaye marehemu Nyaisanga alikuwa meneja wa kituo hicho Abed Dogoli amesema kuwa marahemu alifariki dunia Octoba 20 saa 1 asubuhi katika hospitali ya Mazimbu manispaa ya Morogoro na taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa Marehemu Kihonda na wanatarajia kumsafirisha kwenda nyumbani kwao mkoani Mara kwa ajili ya maziko.
No comments:
Post a Comment