Ile mkuu wa wilaya ya
Bahi Betty Chalamila Mkwassa anaingia studio tu, akalakiwa na nduguye Paul
James Sweya, hawajaonana siku nyingii, furaha iliyoje waooo! walikua wanasikilizana kwa mbaliii!
Wilaya
ya Bahi ina kata 21 ,ka ujumla wanakijiji laki 225,156
,
na kila kata ina kamati ya watu 6watakao hamasisha ujenzi wa hospitali ya
wilaya na .mwenyekiti ni mkuu wa wilaya ya bahi bi betty chalamila mkwasa.
Hospitali
nitakua ni ya ghorofa, ujenzi unatakiwa kuanza january mwakani na itagharimu 1
bilioni nukta nane
Wananchi
wa bahi ni wagumu kutoa pesa ni heri akupe mifugo, hilo mkuu wa wilaya
amelikubali, atawahamsisha wafugaji wakubwa watoe ng’ombe,kondoo,mbuzi,kuku
watauza ili kupata fedha za ujenzi.
Wenye
vifaa vya ujenzi watoe si lazima sana fedha la hasha, mkuu wa wilaya ya bahi
mpaka mwakani anategemea kupata milioni 800 ili kuanza ujenzi huo.
Baada
ya kukamilika kwa ujenzi, utajengwa mnara wenye majina ya walio changia ujenzi
wa hospitali ya wilaya ya bahi.
Wana
bahi walioko mijini wana paswa kuanza kuchangia na wana kamati zao kutokana na
umoja wao ulioko vijijini na jumapili hii wana kutana na december mwishoni wawe
wamekamilisha michango yao.
MGANGA
MKUU DK NTULI
wamefanikiwa
kupunguza vifo vya mama na mtoto mwaka jana alikufa mama mmoja tu , na haya ni moja ya mafanikio
ya kufikia maendeleo ya millennia, mpaka kufikia mwaka 2015 kusiwe na kifo hata
kimoja cha mama na mtoto.
CHANGAMOTO
Wananchi
wa wilaya ya Bahi wanalazimika kutembea umbali wa km 15 kufuata huduma za
matibabu,jambo ambalo ni la hatari ,ujenzi wa hospitali hiyo utakapo kamilika kitaalamu
kutakua na vitanda 350,
matarajio
ni kuwafikia na wananchi wa maeneo ya manyoni
Wilaya
ya Bahi iko barabara ya Dodoma-Singida
hivyo itaokoa watu wapatao ajali maeneo hayo.
BETTY
Alisema kwamba Inakadiriwa
kwamba wa jengo hilo la ghorofa la opd ,ujenzi wake utakamilika kwa muda wa
miaka 2, wagonjwa wanaokuja na kurudi,wanaweza kulaza wagonjwa ikibidi.Na hospitali
hiyo itakua katika makao makuu ya wilaya.
WITO
WA MKUU WA WILAYA KWA WANA BAHI
Mkuu
wa wilaya ya wana bahi, amewataka wana Bahi waungane na kushikana mkono katika
ujenzi huu wa hospitali ya wilaya, na hawawezi kuisubiri serikali kuwafanyia kila kitu wao wataanza na mkuu wa wilaya ana
imani serikali itaweka mkono wake tu. Bahi watahitaji zaidi vitendea kazi,
wadau wengine watafuatwa baadaya ujenzi wao kuanza na january ndo harambee itaanza kwa
uzinduzi.
katika
hili clouds fm imeahidi kua ni sehemu ya mchakato na kueleza maendeleo ya mradi
uliko fikia.big up clouds media group!
Namimi niliona niweke historia vyema, nlifanya kazi na huyu mnayalukolo pale IPP, isee huyu mama ni wa pekee, nafurahi kupiga naye picha kama kumbukumbu.
Madee mmoja ya wasanii watao panda jukwaani jumamosi ni huyu.naye alikuwepo leo mjengoni kwenye power Breakfast.
Madee akiwa amepoz.
No comments:
Post a Comment