Ikiwa bado mixtape yake
“Nyota njema ya mtaa” inaendelea kufanya vizuri sokoni, Chaba a.k.a Baba mkubwa
anayewakilisha 009 (Ngalimited) Arusha city, anawazawadia wapenzi wa muziki
wake track mpya na moto kabisa toka Grandmaster Records chini ya utayarishaji
wa producer John B akiwa amemshirikisha Jordan aliyetisha na ngoma yake ya
mapenzi vita mapema mwaka huu.
Huyu hapa ni Chaba
akiizungumzia track yake mpya;- “Mmmmh! Hii track basically, ni zawadi kwa
mashabiki zangu kwa kuipokea vizuri na kuinunua mixtape yangu ili pia wasio
nazo waendelee kuinunua, na pia bila kusahau kuwa kawa bado Baba mkubwa
nawa-murder rappers wote wanaoigiza sanaa”
No comments:
Post a Comment