Wednesday, October 31, 2012

TANESCO

UKISTAAJABU YA MUSA! UTAYAONA YA FIRAUN


Wakati Wa Tanzania tulipata mshtuko kusikia kua wasomali ama wahamiaji haramu wengine huingia Tanzania kwa usafiri wa mafuso wenzetu hutiwa ndani ya majeneza ama bath tabs na kusafirishwa kama mizigo mradi wafike waendako! lakini safari hii wawili ama watatu wamedakwa! mbwa kunusa ndiye aliyegundua!

maofisa wanakiri kwamba mara zote walikua wakitumia vifaa vya ukaguzi kukagua mizigo lakini this time round! ni Mitzy mbwa aliyewasaidia kugundua aina hii mpya ya usafiri! POlisi wa Tanzania mpo? kila uchao watu wanabunimbinu mpya! mjipange, hii sio bongo! well mida hii naelekea Shinyanga vijijini katika kijiji cha ITIRIMA kuna mambo huko! wee acha tu jioni ntakuhabarisha! TUWE SOTE MIDA MIDA BASI!

INJINIA MANYANYA AJITOSA KUTETEA NAFASI YAKE YA UJUMBE WA NEC TAIFA KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Injinia Stella Martin Manyanya ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, MNEC Jumuiya ya Wazazi toka mwaka 2007, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mjumbe wa SADC PF na Msimamizi wa Kimataifa wa Uchaguzi kupitia vionjo vya Uhandisi, Ujasiriamali na Sanaa alivyokuwa navyo ameamua kujitosa tena kwenye uchaguzi wa kutetea nafasi yake ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Jumuiya ya Wazazi katika uchaguzi utakaofanyika kesho tarehe 31/10/2012 Mkoani Dodoma

Tuesday, October 30, 2012

HONGERA ARNOLD KAYANDA!

KWANZA NAOMBA RADHI KWA WADAU WOTE WA BLOGG HII, KWAKUCHELEWA KUTUPIA PICHA ZA HARUSI YA KAKA YANGU ARNOLD KAYANDA, KWASABABU JUMAPILI NILIFANYA SAFARI DAR TO SHY TOWN SO NIKAFIKA JIONI SANA NIKIWA HOI, JANA JUMATATU NIKABANWA HATARI, SO HII NI ALFAJIRI WALAU NITEKELEZE WAJIBU NA NIMTENDEE HAKI KAKA NA WIFI YANGU ANITHA RUHINDA! NA HIZINDIZO PICHA NLIZOPATA KWA UCHACHE. ASANTE


           
Hapajicho ni kwa bi harusi popote uendapo na kiukweli wifi ali shine muno! safi sana ndo maana nikaanza naye.mrembo,mchesi,natural hakika kaka kapata jiko hahaha lol.

Maharusi wakikata keki yenye umbo la jahazi kipindi anachofanyia kazi bwa harusi Arnold lakini pia keki zingine zina maumbo ya vikapu ya asili maarufu sana huko Rwanda kama vikapu vya siri! hongera sana Angela Msangi mwandishi habari aliyegeukia ujasiriamali wa keki, kazi zake ni nzuri sana.

Monday, October 29, 2012

OXFAM YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI SHINYANGA

 ALASANA MKUFUNZI AKIJIANDAA KUTOA MADA
 HII NI CHAI YA JIONI
 ILI WATU WASILALE KWENYE MAFUNZO, LAZIMA KUFANYA MAMBO KAMA HAYA!

Sunday, October 28, 2012

UGONJWA WA MARBUG UBAUA KWA ASILIMIA 70-90

Hapa ni nchini Uganda wataalamu wa Afya wakinyunyiza dawa mahali ambapo wagonjwa wa Marbug walitelekezwa hadi kufa, baada ya kugundulika wana ugonjwa huo.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


 

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA.

TAHADHARI YA UGONJWA WA MARBURG
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), tarehe 20 Oktoba, 2012 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda. Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kabale, Kanda ya Kusini Magharibi ya nchi, na wilaya hii inapakana na Rwanda. Mpaka tarehe 24 Oktoba 2012, takriban watu 13 wamepata maambukizo na 6 wamepoteza maisha..

Thursday, October 25, 2012

Usajili wa mbio za Rock City 2012 wasogezwa mbele

                                                                            Picha ya Maktaba

WAANDAJI wa mbio za Rock City Marathon 2012 wametangaza kusogeza mbele usajili wa kushiriki mbio hizo mpaka Oktoba 26 ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki katika mbio hizo.  Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa mbio hizo toka kampuni ya Capital Plus International (CPI), alisema kuwa wameamua kusogeza mbele usajili kutokana na namba ya waombaji kuendelea kuongezeka ili kushiriki mbio za mwaka huu.

MUSTAFA HASSANALI KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA UBUNIFU WA MAVAZI AFRIKA YA KUSINI MWEZI HUU



                                               Mustafa Hassanali

Mbunifu maarufu wa mavazi kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali ndiye Mtanzania pekee katika fani ya mitindo aliyepewa mualiko wa kushiriki katika maonyesho ya Wiki ya Mitindo Afrika chini ya African Fashion International (AFI) yatakayofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 24-28 Oktoba, 2012  katika ukumbi wa Melrose Arch, jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini.

Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya kutengeneza Magari ya Mercedes-Benz yanatarajiwa kuwashirikisha wabunifu wa mavazi zaidi ya 35 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika, baadhi ya nchi hizo ni wenyeji Afrika ya Kusini, Ivory Coast, Morocco, Msumbiji, Cameroon, Rwanda, Angola, DRC, Nigeria, Ghana na Tanzania.


HAMKANI SI SHWARI ARUSHA!


INASEMEKANA KUA KATIBU MKUU WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA, AMERIPUKIWA NA BOMU! WACHA TUFUATILIE!

MAADHIMISHO YA MIAKA 67 YA UN DAR-ES-SALAAM


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta  akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za  maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa nchi za bara la Afrika kutathmini na kupima mafanikio ya malengo 8 ya millennia pamoja na kuongeza juhudi katika kupambana na umasikini na janga la njaa.


 Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akitoa salaam za Umoja wa mataifa wakati wa maadhimisho ya 67 ya Umoja huo jijini Dar es salaam.

MKUTANO WA KWANZA WA UMOJA WA VYUO VIKUU



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wednesday, October 24, 2012

UVCCM WAPATA VIONGOZI




MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe.JUMA SADIFA-2012-2017

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI
Mhe.MBONI MHITA


WAJUMBE NEC
Jery Slaa
Deo Ndegembi
Anthony Mavunde
Jonas Nkya
Kutokea JF

KITCHEN PARTY GALLA PART II

juzi niliahidi kukuletea hizi picha zilizosalia, lakini naomba radhi jana nlitingwa mno, so kiduchuu zilizobaki hizi hapa.Huyu ni Chriss Mauki mwanasaikolojia anayechukua masters yake South AFrica juu ya mahusiano, na usione karatasi alizoshika ndogoooo, ukadhani hamna kitu! eh umesahau kua hamna hamna ndimo mliwamo? alitisha kiukweli i wish kama wanaume wangekuwepo ili nao wamsikie Chris maana alikua anatoa vitu halisi katika maisha ya kila siku. wow! congrats brother.
Getrude Mungai na Chris walikua kama watani wa jadi siku hiyo! na haya mazoezi ilikua ni katika harakati za kuwafanya wanawake wawavutie wenza wao , na practice make it !? PERFECT sio? eeeh ndo maana yake.tulifanya mazoezi mengi na kushare mengi kati ya Mambasa ya Mambasa na Bongo! chezea mapenzi weye? utalia kilio cha mbwa mdomo juu oh! shaurilo kaza buti, simamia mwanangu ahahahaha.
Getrude Mungai sexology, ana ngozi nzuri na ni mzuri pia, lakini pengine mbali ya kula,kulala pazuri,nguo bora, wataalamu wa mambo ya mapenzi wanasema kua usipofanya sex vya kutosha unakua na msongo,mgomgo kuuma,kichwa kuuma na ngozi husinyaa, lakini ukiipata kwa wakati na ukatosheka abhaaaaas! utakua nyororoooooooo!


vifalio kama hivi vilivyoletwa na bi Getrude vilihamasishwa kutumika wakati wa chakula cha usiku kwa wakubwa tu! na yeye alitwambia ana kijitray chumbani kwake kilichofurika vikorombwezo vya kuchokolea pweza mwambani na mashallah kufanikiwa mno, ikiwemo kumfanyia vituko laazizi wake kwenye mtoko wa jioni na laazizi anapotaka kuhakiki anakuta kweli! anapagawaje? hahaha asante mama

MIRADI YA MAJI: DC AMPA SAA 24 MKUU WA IDARA KUMPA RIPOTI

              Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akizindua mradi wa maji

            Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akihakiki kama maji  yanatoka!


                          haya sasa kazi kwenu, maji ndo haya tunakutwisha!

PAMOJA NA HAYO!MKWARA MZITO UMECHIMBWA

Tuesday, October 23, 2012

KWA MNAOPENDA MAVAZI

Nguo hii ni nzuri sana! ila naongeza ubunifu kidogo, kwamba kwa sisi waa Africa ingekua ya kitenge kizuuri itakua tamu sana sio?

NAPENDA KIPEPEO JAMANI,WANAFAIDA !

Utitiri wa vipepeo huu umeonekana Chincua reserve in Mexico, napenda kupiga picha ,sikupigwa lakini hata za kupiga sijaweza vyema mnivumilie.

Inapendezaje? waone walivyokaa inavutiaje?
Idadi kubwa ya vipepeo kama billion hivi huruka kila mwaka baada ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa katika miezi ya October na  March na hufanya safari ya mile 25,000 ili kufuata ujoto joto mahali pengine baridi iwazidiapo!.
 

UAMSHO MAHAKANI WASOMEWA MASHTAKA

Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.

Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.

Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi

RAIS KIKWETE KATIKA KILELE CHA MKUTANO MKUU WA UWT DODOMA



Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
             Mwenyekiti wa UWT mheshimiwa Sofia Simba akiongea jambo lililo chechemua meza.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

VIFAA VYA KUFUNDISHIA VINAHITAJIKA

 Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia

 Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeremia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yesaya (AY).  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia

Monday, October 22, 2012

Mh. Lowassa katika uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya VOCOBA jijini Dar




Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.


Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.

   
                                       Burudani ya Ngoma za Asili.

WOMEN IN BALANCE YAPATA MWITIKIO NA YAFANA SANA!!!




Kiukweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, women in balance Kitchen party gala ilinoga mno! Mi nilikuwepo, watu walifurika na kupitiliza! Na hii ni ishara nzuri kwamba mkutano huo umekua na pnahitajika juhudi za dhati tena za makusudi kuiimarisha ili kuwakomboa wanawake na wanaume katika fikra mgando zinazoyumbisha ama hata kusambaratisha ndoa zao! 



Watu wakaanza kuingia! Huyo mwenye skirt ya orange na blaizer nyeusi ni Babra Hassan wa Power Breakfast  Clouds Fm


Ukaguzi ni muhimu popote pale, basi ilibidi subra ili ukaguliwe! Na mdada white ni Mrs Urio


                        Nyomi lilikua hivi! Na huu ni upande wa kushoto wa jukwaa! Walifurika babake

Friday, October 19, 2012

AT aka MFALME WA MDUARA Feat. DEPLAZIR LIVE ON STAGE @ THE CHAPLE LOUNGE LONDON 3 NOVEMBER 2012.




AT aka Mfalme Wa Mduara feat Deplazir Live on Stage @London The Chapel Lounge ig1 2af Sat 3rd November One Show Only..! Hosted By BongoDeejays |Chriss Luv Promotion| Jestina George Blog, So Get Your OutFit Ready Let Make it Happen Catch you there..! 

IT'S A BLACK & WHITE AFFAIR!!!
SO TELL YOUR FRIEND TO TELL A FRIEND

UNDP YAIPONGEZA TANZANIA KWA JITIHADA ZA MAENDELEO




 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye kukuza uchumi.