Friday, September 28, 2012

"Afanya mapenzi" na magari 1000



Sijui ni wazimu au nikupagawa ?.Lakini Edward Smith  kutoka Washington Marekani anasema yeye ni Mzima na akili zake.

                                                                  Edward Smith


 Edward Smith hana haja na mpenzi anayetembea kwa miguu miwili.Mmarekani huyo anasema sio hata hana hisia , anazo tena nyingi. Lakini sio kwa binadamu.
Edward Smith ambaye ni mtunzi wa mashairi ana fanya mapenzi na gari, kufanya mapenzi kwa maana halisi ya kufanya mapenzi . Smith anasema akiwa na hamu hufanya na gari kama vile nissan, pudjo, mercidez benz na vitu kama hivyo, lakini sio mtu.

The Rise And Rise Of Matata Fahari ya Tanzania!!!

Flaviana Matata (© Facebook) 


Africa ni sehemu pekee ambako ma models hukuzwa kuanzia level ya chini hadi kufikia kiwango cha juu, nah ii ni kwa miaka mingi iliyopita na kufanikiwa kuchangia ukuaji wa biashara models.
katika miaka ya hivi karibuni, maonesho kadhaa ya mavazi ambayo huendeshwa nje na ndani ya bara la Afrika basi hukosi kuwashuhudia models wa bara kubwa Africa!
 
Flaviana Matata (© Facebook) 


Model Flaviana Matata,  kutoka nyumbani Tanzania ana umri wa miaka 25 , na anajulikana kimataifa kwa kazi zake zilizotukuka za modeling  na kujinyakulia sifa ya becoming one of the world’s brightest stars.

Wednesday, September 26, 2012

KATY PERRY NDIYE BILLBOARDS WOMAN OF THE YEAR

Cast member and singer Katy Perry poses during a photocall before the premiere of ''Katy Perry: Part of Me'' in Rio de Janeiro July 30, 2012. REUTERS/Ricardo Moraes


Pop star Katy Perry  ametajwa jana kwamba ndiye mwanamke aliyefanya vizuri sana katika chati za Billboard's  na atapewa tuzo ya Billboard's Woman of the Year, nah ii ni baada ya kung’ang’ana kwenye chati hizo kwa miezi 12  na huo ndio wakati amabao alikua ametalikiana na mumewe na alihit katika single na filamu  .
Perry, mwenye umri wa miaka  27, alitalikiana na mumewe mwenye asili ya Uingereza mchekeshaji   Russell Brand  mwishoni mwa mwaka wa jana na wakati huo single yake ya "Part Of Me" ilikua juu ya chart hizo na   filamu ya 3D  ya behind-the-scenes ikimuonesha "Katy Perry: Part Of Me"  ambayo inayahusu maisha yake kitaaluma kupanda na kushuka ikiwa ni pamoja na mahusiano yake.
Ushindi wake umeanzia kwenye ukurasa wa mashabiki wake katika kurasa za Twitter na Facebook  ujulikanao kama katycats na vilivyompa umaarufu ni  costumes zake na  bubble gum pop songs.
Jarida la Forbes  limempaisha Perry katika nafasi ya 3  kati ya wanawake wanamuziki wenye mkwanja mrefu mpaka kufikia December 2011, inakadiriwa kua alikua ana mkwanja wa dola milioni 44.

ULAYA YASITISHA MSAADA KWA RWANDA

Bendera ya Muungano wa Ulaya 

Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi wananchi.Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.

Maradhi yanayosababishwa na matango hayajawahi kushuhudiwa

Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi. 


Watalaam wa afya nchini Ujerumani wanasema kuwa maradhi yanayosababishwa na matango ni bakteria wapya, na wanaweza kuathiri maini na damu ya mtumiaji.
Backteria hao ambao wamezuka huko Ujerumani na Sweden hadi sasa wamesababisha vifo vya takriban watu 18 na zaidi ya watu 1500 wameathiriwa na backteria hao baada ya kula matango hayo.

Tuesday, September 25, 2012

Mahaba ya Dhati Yamvua Nguo Mume

Njeru man caught stealing, forced to strip 

Tama za Mke  zamsabishia mume adhalilishwe

Wafanya biashara wa   eneo la GOKHALE  nchini Uganda walikua wakiendelea na shughuli zao za kila siku huku wakimshuhudia mwanamume mmoja akiwa mtupu huku akiisukuma baisikeli yake na miguuni ana soksi zake!
Mwanamume huyo alilazimika kutembea mitaani akiwa utupu baada ya kukamatwa akidokoa body lotio kwenye supermarket moja. 

Monday, September 24, 2012

Rais wa Zamani wa Zambia Akumbwa na Kihoro

Kenneth Kaunda hospitalised 

Rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda 

Rais wa zamani wa Zambia  Kenneth Kaunda jumamosi iliyopita alilazwa hospitalini katika hospitali ya University Teaching Hospital  kutokana na ugonjwa uso julikana ama pengine niseme kihoro na kusababisha ibada ya maziko ya mkewe iahirishwe! Na huo ni uamuzi wa familia yake,
Mke wa Rais huyo wa Zamani wa Zambia bibi Betty alifariki jumatano ya wiki ilokwisha akiwa na umri wa miaka 83 akiwa nchini Zimbabwe ambako alikwenda kumtembelea binti yake. Na maafisa wa serikali wanaeleza chanzo cha kifo chake kwamba alifia usingizini nyumbani kwa binntiye aitwae Musata Kaunda-Banda  katika jiji la Harare eneo la Borrowdale Brooke.

Friday, September 21, 2012

HIZI NDIYO SABABU 25 ZA KUIPENDA AFRIKA





Boy in sunglasses (© Flickr/p r o m i s e)

Africa ndilo bara la pili kwa ukubwa duniani. Bara hili lina ukubwa wa  square kilometers milioni 30 , na haliko mbali na bara la Asia lenye square kilometer milioni 44 . si hay ohayo tu kuna Marekani,China  na India yanayoingia bara Asia na kuunda  European countries.
Boy in sunglasses (© Flickr/p r o m i s e)

Najua mlio wengi mnazijua  pyramids zilizoko  Egypt tu! Lah hasha bali zipo pia  North na South Sudan. Na kwa ujumla wake nchi hiyo ina  pyramid zaidi ya 220 pyramids na ni za zamani kuliko za  Egypt. 

Thursday, September 20, 2012

Wimbo Bora Wa Gospel Africa 2012




Anaitwa Emmy Kosgei kutoka kule Kenya, yeye ndiye mshindi kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka kwenye tuzo za "Africa Gospel Music Awards 2012" zilizofanyika huko Uingereza.. Tuna mengi ya kujifunza ili tuweze kuwa "VICHWA"  na sio mikia, kama una amini sema AMEN! BARIKIWA..

Keki Yamtisha mtoto




siku ya kuzaliwa kwa kila mwanadamu ni siku muhimu sana katika maisha, kwani ndiyo siku uliyoingia duniani kwa mara ya kwanza!
niangalie upande wa watoto, wapo ambao hufanyiwa birhtdays kwa namna tofauti tofauti! sura huchorwa, hupelekwa mahali kula apendacho! ama hupewa nafasi ya kuchagua zawadi aipendayo kwa familia zenye uwezo!
lakini moja ya zawadi apewayo mtoto mbali na zingine zote,  ni keki zenye maumbo mbalimbali, sasa! kwa wale wenye ufahamu mdogo hupewa keki ambazo wakati mwingine huwa zinawatisha! tazama hii!

Wednesday, September 19, 2012

Aina 5 Ambazo Wanawake Wanafanya Vizuri Zaidi



Leaders

Wanawake walio wengi hukumbana na vikwazo lukuki wakiwa kazini tofauti na wanaume wao mambo hua shwari! Lakini pamoja na vikwazo na yote atakayopitia mwanamke! Moja lililokuu ni kwamba uwezo wake kiutendaji ni mkubwa pengine kuliko wanaume, na heshima huwa juu zaidi pale tu mwanamke anapokua na cheo kazini, hapo kila mwanaume huweka heshima.

Tuesday, September 18, 2012

Mwaka wa Taabu na Misukosuko kwa Lauryn Hill



Ex-Fugee: Hill's baby daddy was actually Bob Marley's son Rohan
Lauryn Hill



Mwanamuziki Wyclef Jean amefunguka na kuachilia lawama za kufa mtu kwa mzpenzi wake wa zamani ambaye pia alikua nae kwenye bandi moja,  Lauryn Hill yakwamba alimdanganya juu ya mtoto wa kiume ya kwamba ni wake kumbe sivyo
Kutokana na hilo Wyclef anajiona ametendwa! Na kugeukwa kusiko weza kusameheka , na lawama hizi za Wyclef Jean  zimeibuka na kutonesha madonda na kutupia kwenye kitabu alichoandika juu ya Lauryn Hill akidai  kua ndiye baba wa mtoto wake, kumbe LONGO! 

Monday, September 17, 2012

Waziri Mkuu wa Zimbabwe apata Jiko!!

Morgan Tsvangirai marries his wife, Elizabeth Macheka amid controversy, in Harare. 

 Ni raha tele! bwana na bibi Tchangirai

WAziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amefanikiwa kufunga ndoa yake siku ya Jumamosi licha ya mahakama ya nchini mwake kumzuia kufanya hivyo!
Na hii ni baada ya mke wa kimila kupeleka mashtaka mahakamani na kudai kwamba wao bado ni mke na mume halali, kwa mila na desturi za kabila lao na sheria za kabila hilo.mahakama hiyo ilielezwa kwamba waziri mkuu huyo Morgan Tsvangirai alilipa mahari juu ya mwanamke huyo mwaka wa jana na kumuoa!

Friday, September 14, 2012

Maandamo Dhidi Ya Filamu Ya Kuukashifu Uislamu Yasambaa



 Maandamano dhidi ya filamu ya kumkashifu Mtume Muhammad mjini Tunis, Tunisia.

Maandamano ya Waislamu yameenea sehemu nyingi duniani wakipinga filamu iliyotengenezwa Marekani na inayomkashifu Mtume Muhammad, ambapo polisi wa Cairo wametumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji hao.

Rais wa Muhammed Mursi wa Misri ametoa baraka za kufanyika kwa maandamano ya amani lakini akasema ni kinyume kuwaua raia na kushambulia balozi. "Kutoa maoni, uhuru wa kuandamana na kutoa misimamo ni jambo ambalo linakubaliwa lakini pasipo kuharibu mali na balozi." Amesema Rais Mursi kupitia televisheni ya nchi yake huku pia akilaani mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya na kuahidi kulinda wageni.
Wizara ya afya ya Misri imesema watu kumi na tatu wamejeruhiwa katika maandamano hayo ambapo waandamanaji wameshusha bendera ya Marekani na kuichoma na kisha kupandisha bendera nyeusi.

Klabu ya waandishi wa habari Iringa yasitisha ushirikiano na polisi.

 

Klabu ya waandishi wa habari mkoani  Iringa –IPC nchini Tanzania, kwa kushirikiana na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani  humo,  kuanzia Jumanne imetangaza kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi la polisi mpaka pale taarifa au majibu sahihi kutoka vyombo huru zitakapotolewa kujua aliyemuuwa mwandishi wenzao Daudi Mwangosi wakati wa vurugu za chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema na polisi.

Thursday, September 13, 2012

Sad News:Nonini na One FM wajitolea kumsaidia bondia wa kike aliyewehuka





Bondia bingwa mwanamke wa Kenya Conjesta Achieng tarehe 24 mwezi Desemba alimshinda mchezaji kijana wa Argentina Guillermina Fernandez bila kutumia nguvu nyingi na kupata ubingwa wa ngazi ya uzito wa katikati kwa wanawake wa shirikisho la ndondi duniani IBF baada ya kupata mkanda wa dhahabuwa baraza la ndondi la kimataifa WBC.




Katika mchuano huo wa kumtafuta bondia bingwa mwanamke, nguvu bora ya Conjesta Achieng ilionekana dhahiri, dakika 1 na sekunde 40 baada ya kuanza kwa pambano hilo, alifanikiwa kumweka Guillermina Fernandez kwenye kona kwa mashambulizi makali na kumlazimisha kocha wa Fernandez apeperushe taulo na kuonesha kushindwa.
Ushindi wake dhidi ya Fernandez umefanya jumla ya mafanikio ya Achieng yawe kushinda mara 21 na kushindwa mara 3. Mchezo huo ulifanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Kenya ambao ulichelewa kufanyika kwa saa tano na kusababisha malalamiko kutoka kwa watazamaji. 

 





Conjesta alipewa jina la utani la ‘hands of stone’ kwa uwezo wake wa juu kwenye ndondi. Ni mkenya aitwaye  Conjestina Achieng’. Habari mbaya ni kuwa boxer huyu wa kwanza wa Afrika kuwahi kushinda taji la dunia amekuwa chizi.

Uchizi wake huu umetokana na kuvuta bangi na ulevi wa kupindukia. Kwa sasa anaishi na dada yake kwenye chumba ambacho ameshindwa kukilipia kodi kwa miezi minne.

Rapper wa Kenya Nonini akishirikiana na kituo cha radio cha One Fm cha Nairobi, Kenya na Bernsoft Interactive Present ameanzisha kampeni iitwayo PAMOJACONJE2012 INITIATIVE ili kumchangia fedha bondia wa zamani Congestina Achieng aliyewehuka.

Kupitia Facebook, Nonini ameandika:

“Ni initiative imeanzishwa na Nonini ku support Congestina Achieng boxer wetu wa nguvu! Kuna ile story that ran on TV and is on Newspapers all over about her current Health.The Initiative is very Transparent because we have blessings of Conje’s Dad Clement Adala and the sister who currently lives with her Caroline Adala. They are Signatories to the Account that has been opened at Family Bank.

Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Ulipofikia



ujenzi wa daraja la Kigamboni ulipofikia ambapo linaendelea kujengwa katika bahari ya Hindi,eneo la Kurasini jijini Dar-Es-Salaam, ambapo likikamilika litakua na njia zipatazo 6 ,zikiwemo barabara za juu na likikamilika litakua daraja kubwa na la kipekee  katika nchi za Africa Mashariki na Kati.






Mmoja wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye mtando unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo
au nyaya zinawajua wakandarasi?  so haziwadhuru? hahahaha lol.

Ziara Ya Prince Williams na Mkewe Cathrine


Prince William na mkewe Catherine  walipewa mapokezi wanayostahili pindi walipowasili nchini Singapore  mnamo siku ya Tuesday  siku waliyoanza ziara ya siku ya kuzunguuka  kusini mashariki mwa Asia na Pacific ya kusini
Wawili hao wenye mvuto wamo katika maadhimisho ya miaka 60  ya   anniversary ya malkia  Elizabeth na mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege moja kwa moja  akaelekea katika viunga vya bustani ya maua ya Singapore Botanical Gardens  mahali ambapo walipewa zawadi ya ua nono aina orchid ambalo chotara . lakini pia katika bustani hiyo Prince Williams alipata kumbukumbu ya mamake mpenzi pale alipooneshwa ua aina hiyohiyo ya Orchid lililopewa jina la mamake mzazi  Princess Diana

Historia


               miaka milioni 130 iliyopita nyoka walitokana na mijusi! upo?


                                                              chanzo cha nyoka

Malimwengu!!



Mwanaume akipita mbele ya kiti chenye urefu wa mita 6.8 sawa na futi 22 na upana wa mita 7.7 sawa na futi 25 kilichoko katika shopping mall  nchini China katika mji wa Shanghai. kiti hicho kimetajwa rasmi kua ndicho kikubwa zaidi duniani.

Wednesday, September 12, 2012

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI KUPINGA KIFO CHA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI


Mhariri Mkuu wa NIPASHE, Jesse Kwayu akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya David Mwangosi (katika picha kulia) kwenye viwanja vya Jangawani, jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo



Waandishi wa habari wakiandamana  kuelekea viwanja vya Jangwani, Jijini Dar-Es-Salaam.



     Waandishi wa habari wakiandamana  kuelekea viwanja vya Jangwani, Jijini Dar

Tuesday, September 11, 2012

Google Kushtakiwa Kwa Upotoshaji!



                                                                   Bettina Wulff

Mke wa rais wa zamani wa Ujerumani ameazimia kuishtaki kampuni ya GOOGLE mahakamani kufuatia kampuni hiyo   kueneza uvumi wa maisha yake binafsi katika mtandao..

Picha kama hii ilikua kwa matumizi yake, ninyi mitandao vipi?

Mke wa rais huyo aitwae WULF BETTINA  amesema ukilitafuta jina lake katika GOOGLE  linatoa majibu kwamba jina hilo ni la mtu ambaye ni kahaba  aliyekubuhu katika mitaa mbalimbali  nchini humo.
Bi WULFF amekanusha kwamba yeye hakuwahi kufanya kazi hiyo ya ukahaba  na  ameahidi kutoa tamko  katika gazeti moja la kijerumani  kwa ajili ya kukanusha madai yote yanayohusina na yeye kufanya kazi ya ukahaba  kabla ya kuolewa.

Friday, September 7, 2012

Je? Jina La Babako Lina Maana Gani? Linakutoa? Soma hii!!



                                                Ini Edo
Iniobong Edo naweza kutamka kwamba pengine ndiye msanii nguli zaidi kutoka katika eneo la Akwa Ibom jimbo ambalo ni eneo la mafuta la Niger Delta  ,nchini Nigeria! Lakini! Kuna jambo kwa nguli huyo katika kichupa Africa ya Nolywood hadi Hollywood, nini unajua? Jina lake lina mambo
Kwa wanaomjua nguli huyo! Wanadai kwamba!  Edo sio jina lake na pengine alilionea wivu jina lake la asili la baba yake mzazi na mzazi anashangaa alikolitoa jina hilo , na taarifa za kulikana jina hilo la Edo zimetoka ndani ya familia yake tena mtu wa karibu yake sana!.



                                             
                             Ini Edo kimtindo

na mtu huyo aliapa na kuapa kwamba! Babake japokua hapendezwi na hilo, lakini hana la kufanya, ndo mwanawe na kama haitoshi ni maarufu nchini Naijeria na dunia kwa ujumla, lakini hana amani naye na haelewi sababu za msingi  za kukana jina la babake na pengine ameliona halimfai kwasababu yeye ni mashuhuri kwa sasa!


 
                                          babake Ini Edo                               

jina la babake halisi ni Ekim likiwa na maana ya (Darkness) giza kikwao sasa!inasemekana ,Ini  Wakati akihangaika kutoka kwenye tasnia ya maigizo akawa na imani ya jina hilo kua na maana ya nyeusi ama giza halitamtoa! Basi akachukua hatua na kuling’arisha jina hilo la darkness na  kujiita Unwana hahahha likiwa na maana ya (Light) ok! Mwanga .lakini baadae akashauriwa na baadhi ya marafiki zake kutafuta jina ambalo litawashika mashabiki na kutamkika kirahisi kwenye tasnia!

 
       Ini Edo katika muonekano wa kichavi chavi! lol

Na hatua zaidi ilikuja baada ya kugunwa na hata kushangaliwa kwa jina lake jipya tena Unwana  akaona isiwe taabu akajiita jina la pili Edo  ambalo kwake yeye aliliona tamu na rahisi kutamkika na halitakua na nasaba yoyote na kiza ama niseme darkness tena

                            Ini Edo ki africa zaidi

Inawezekana kwamba hilo ndo lilikua ndo jina lake la bahati kwani lilifungua milango mingi ya mafanikio kwake ,ingawa hakuna mwenye uhakika jina la babake linge mbwaga chini