NI dhahiri kuwa vipaji vikiibuliwa tangu utotoni na
kuendelezwa vyema vijana wanakuja kuwa wazuri ukubwani na kulitangaza vyema
taifa nchi za nje.
Hali hiyo inadhihirika kwa kijana Ibrahim Class 'king Class
Mawe' ambaye anafanya vizuri katika medani za ngumi ambazo zinamsaidia kuinua kiwango chake.
Tangu aingie katika mchezo huo ameshiriki katika mashindano
mengi na kufanya vizuri na kusababisha wadau mbalimbali wa masumbwi kumtabilia
kufika mbali mbali ikiwa atazingatia mazoezi.
King Class anasema alishawishika kuingia katika mchezo huo
kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo tangu utotoni ambapo alikuwa na ndoto za
kuwa mwanamasumbwi.
Anasema kuwa ndoto yake ilianza kutimia baada ya kaka yake
naye anaeitwa Chaku Master kuwa mwanamasumbwi alikuwa akifanya vyema miaka
kadhaa iliyopita.
Chaku nilikuwa nikiishin naye hivyo wakati anakwenda kufanya
mazoezi nilimuomba kuongozana na hali iliyonifanya kuanza kucheza licha ya kuwa
ni ndoto yangu ya siku nyingi, anasema King
Class.
Kocha wake wa kwanza kufundisha kucheza ngumi alikuwa ni
mzee Babu Tule ambaye alimpa misingi ambayo inamfanya hadi kuwa bondia mzuri
anaeshimu nidhamu na sheria za mchezo huo.
Mwaka mmoja baada ya kuwa na kocha huyo alimuamishia kwa
kocha Mkongwa Habibu Kinyogoli ambapo
hapo alikutana na makocha wengi akiwemo kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa
Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
ili kumpa mbinu zaidi za mchezo huo na kumjenga katika misingi thabiti
ya kufikia ndoto za kifikia mafanikio.
Anasema mwaka 2006 baada ya kuwa chini ya kocha wa siku
nyingi katika mchezo huo Kinyogoli kiwango chake kinakuwa kikiongezeka kila
siku na kuwa tishio katika ngumi za amacha.
Class anasema tangu wakati huo amepambana mapambano mengi
ambao alifanya vizuri na kumbukumbu yake inaonesha alifanikiwa kuwatwanga
wapinzani kwa KO katika mapambano zaidi ya 10, ndicho kitu anachojivunia kwa
sasa.
"Huwa najisikia faraja ninampompiga mtu kwa KO kwani
inazidi kunijengea heshima katika ngazi
ya amacha ambayo ndiyo niliyopo kwa sasa ambayo nahisi sina mpinzani,"
anasema Class.
Anasema siri kubwa ya kufanikiwa kufanya vizuri katika
mapambano yake ni kutokana na kuzingatia mazoezi, miiko, sheria na kanuni za
mchezo huo ambazo kila siku huwa anaelekezwa na kocha wa Kinyogoli.
Chipkizi huyo katika masumbwi anasema kila bondia
anaweza kufanya vizuri ikiwa atajihidi
kusimama imara kuzingatia yanayokatazwa katika mchezo huo.
"Moja ya vitu ambavyo avitakiwi ni uvutaji wa sigara na
utumiaji wa dawa kulevya ikiwemo Bangi na dawa nyingine ambazo ufanya kuwa na
uhamuzi usio sahihi," anasema Class.
Class anasema ikiwa bondia atatumia Sigara au akivuta bangi
ufanisi wake unakuwa mdogo kutokana na kifua kuwa kizito na kushindwa kumaliza
raundi za mchezo au anaweza kupigwa kwa KO.
Hivyo anawashauri mabondia ambao wanajihusisha utumiaji wa
tumbaku kuhachana na tabia hiyo ili kufikia malengo waliojiwekea katika
masumbwi.
Pia unywaji wa pombe nayo ni sehemu
inayonyong'onyesha viungo, ikiwa bondia atahitaji kufanya vizuri ni vyema
akaepiuka utumiaji wa pombe.
Kingine anasema kuwa suala la uzinzi nalo ni tatizo kwa
baadhi ya wanasumbwi na ndiyo sababu kubwa inayowafanya kushindwa kufanya vyema
ulingoni na kuambulia kupigo kikali.
Hivyo anawaomba wanamasumbwi chipukizi na wakongwe
kujiepusha na hanasa hizo ambayo zinarudisha nyuma harakati za maendeleo ya
mchezo huo nchini.
Kijana huyo aliyezaliwa
taehe 10/10/1990 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya msingi Mafinga mwaka 2000, mkoani Iringa
anasema licha ya kujihusisha na masumbwi
pia ni fundi wa vifaa vya umeme ikiwemo pasi, TV, Friji,specer na vifaa vyote
vinavyotumia umeme pia ni DJ wa kutumainiwa katika moja ya klabu kubwa jijini
Dar es salaam.
Ili kuundeleza mchezo ni bora vifaa vikatolewa kwenye klabu
mbalimbali zinazoinua mchezo huu kwa vijana wadogo ambao mara wamekuwa
wakitatizwa na nyenzo za kufanyia mazoezi.
King Class Mawe kwa sasa aliemia katika ngumi za kulipwa na
kufanya vizuri katika mapambano yake ya awali ikiwemo kumtwaga bondia Sako
Mwaisege kwa K,O ya raundi ya tatu na kufanikiwa kumdunda bondia mkongwe wa
mchezo huo Jonas Segu na Said Mundiwa Tanga kwa point na kufanikiwa kuweka
rekodi yake ya masumbwi kuwa nzuri
Bondia huyo kwa sasa yupo kambini kwa ajili ya mpambano wake
na bondia kutoka Morogoro Haruna Magali Feb 2 katika uwanja wa Jamuhuri
Morogoro
King Class Mawe kwa sasa yupo chini ya kocha wa kimataifa wa
mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuakikisha kipaji
chake kinakuwa na anapata michezo mbalimbali hapa nchini na matarajio yake ni
kuwa bingwa wa Taifa na bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa Masumbwi
No comments:
Post a Comment