Kutoka Skylite Band Annette Kushaba na Mary Lucas walikua wanahamasisha ulitazame jukwaa kila wakati.
Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM.
Keki ya club bilicanas.
keki ya Clouds fm,
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni
Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi , Monica
Victor na Pili Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja
wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group,Dr Lilian Mtei akikata jikeki
Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas
Group, Dk. Lilian Mtei ambapo
aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992.
“Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea
kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.
Upande
Clouds FM na Clouds TV , iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu
Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa
kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.
Champeign zilifunguliwa za kumwaga! CHEERS.
.
Ikikatwa shurti iliwe! kula Dr Mtei
Wadau nao walipelekewa kuonja.
WADAU mbalimbali wa burudani
walifurahia kwa pamoja miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds
Fm, iliyoambatana na shamrashamra
mbalimbali ndani na nje ya ukumbi huo.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya
Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine.
DR Lilian Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali
waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa
wafanyakazi waliokuwapo tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na
hatimaye kukata keki hiyo.“Uwepo wa
miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa
heshima ya pekee Mama Victor na Mrs
Mitemo ndiyo watakao kata keki hii” alisema
Mtei.
No comments:
Post a Comment