Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya wa Australia.
Muuguzi mkuu wa Idara ya Afya kutoka serikali ya Australia Bi. Catherine Stoddart (kushoto) akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli katika viwanja vya wizara hiyo jijini Dar es salaam. Magari hayo 2 yaliyotolewa kwa msaada wa wadau wa afya wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Austaralia yatapelekwa kusaidia utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli(kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia.
Wawakilishi
wa wadau wa
afya mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia wakiongozwa na Muuguzi
mkuu kutoka Idara ya Afya ya serikali ya Australia Magharibi
Bi. Catherine Stoddart (wa pili kutoka kushoto waliokaa) wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada
ya kukabidhi msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa.
No comments:
Post a Comment