Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni
Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na
Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania
kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa
ndani ya kundi lake la Quartier Latin.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga
akimlaki (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi
Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar
usiku.Mwanamuziki huyo machachari awapo jukwaani ameshuka na skwadi lake zima
la Quartier Latin kwa ajili ya
kutumbuiza siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini
Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,ambapo kiingilio
kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa
shilingi 15,000/= getini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga
akizungumza na (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara
baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar.
Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari
kwenye viunga vya hoteli ya Serena .
Baadhi
ya wadau na wapenzi waliokumbana uso uso kwa na mwanamuziki Koffi Olomide usiku
huu,wakipata picha ya pamoja.
Mdau Idd Janguo nae
alipata picha ya ukumbusho na Koffi Olomide,ambaye anasema amejipanga vyema
kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar siku ya jumamosi ndani ya vuwanja vya Lidaz
Club.
No comments:
Post a Comment