Amin Salmin
Adai si ndugu yao
na hapaswi kutumia jina la Baba yake
MTOTO wa
pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amin
Salmin, ameibuka na kukanusha vikali kuwa 'Ndugu Jambazi' Kassim Ramadhan Juma
(27) aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kukamatwa kwa ujambazi kuwa
si ndugu yao katika familia.
Akizungumza na Mtandao wa
www.sufianimafoto.blogspot.com, Amin, alisema kuwa amesikitishwa sana na kijana
huyo aliyeripotiwa katika vyombo vya habari kwa tukio la ujambazi kwa kutumia
vibaya jina la Baba yake wakati si mtoto wa baba yake na wala hakuzaliwa na
Baba yake na pia na ndiyo maana anaita Ramadhan Juma.
Aidha Amin alisema kuwa wakati mama yake na mtoto
huyo anayejulikana kwa jina la Salma Kasu, alipokuwa akiolewa na Baba yake
mwaka 1990, tayari mtoto huyo Kassim Ramadhan Juma, alikuwepo na alikuwa ana
umri wa miaka, 22 ambapo hadi leo ana umri wa miaka 27.
''Wakati Baba yangu akimuoa Mama yake na Ramadhan
huyu kijana alikuwa na miaka 22, inamaana Baba yangu alimkuta mama yake akiwa
tayari na mtoto mkubwa tu, ambaye Mama yake alizaa na mume mwingine kabla ya
kuolewa na baba yangu,. sasa iweje leo ajiite mtoto wa Salmin tena katika mambo
yake mabaya yasiyofaa katika Jamii, si kutaka kumchafua tu Mzee wa watu na
kumpa mipresha ya bure, baba yangu''?. alihoji Amin.
Kwa kubainisha usemi wake Amin, aliongeza kuwa
anawatambua vilivyo nduguze watatu, aliowataja kwa majina, kuwa ni Abal, Hamoud
na Salama, ambao wamezaliwa na mama wa Kassim Ramadhan Juma, na Baba yake mzazi
Dkt. Salmin Amour.
''Mimi nawatambua ndugu zangu ambao Baba yangu
amezaa na Mama wa Kassim Ramadhan Juma, Salma Kasu, lakini huyu 'ndugu Jambazi'
wala simtambui katika familia yetu, na wala hajawahi kutokea kati yetu kutumia
jina la baba kwa 'Ujina na upuuzi' kama anavyofanya huyo ndugu Jambazi,
Namuomba sana huyo Kassim Ramadhan Juma, na wenzake wasiendelee kutumia jina la
Baba yangu kwa maovu yao kwani ni kutaka kumchafua tu baba yangu ambaye
haitaji kuwa na presha za namna hiyo kwa sasa''. alisema Amin
No comments:
Post a Comment