Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) akiwa mbele ya Kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar Hayati Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja juzi. Rais Wakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk Bilal alifika eneo hilo juzi katika ziara yake ya kuwatembelea wazee mbali mbali mkoani humo,
Makamu akiondoka katika kijiji hicho cha Makunduchi baada ya kuzulu Kaburi la Hayati, Abdulwakil, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa Mzee Ali, Asha Ali Ghulam Hussein.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja.
No comments:
Post a Comment