NAFASI
ZA UFADHILI WA
MASOMO YA SSEKONDARI
KWA YATIMA WA
KIKE
RafikiElimu
FOUNDATION ni Taasisi
isiyokuwa ya kiserikali
inayo jishughulisha na
Maendeleo ya jamii. Taasisi inapenda
kutangaza nafasi za
ufadhili wa masomo
ya sekondari kwa
waombaji wenye sifa
zifuatazo :
1. Awe yatima wa
jinsia ya kike
au awe masichana
anayeishi katika mazingira
magumu.
2.Awe raia wa
Tanzania.
3. Awe
anajiandaa kujiunga na
masomo ya kidato
cha kwanza kuanzia
Januari 2013. AU
4. Awe
anajiandaa kujiunga na
masomo ya kidato
cha tano katika
mwaka wa masomo 2013/14.
5. Awe ni mwanafunzi
ambaye tayari anasoma sekondari lakini
anashindwa/ ama ameshindwa kuendelea
na masomo yake
kutokana na kufiwa
na wazazi ama walezi wake.
* N.B : Ufadhili
wa masomo kwa
kidato cha tano
na sita utatolewa
kwa wanao taka
kuchukua masomo nya
michepuo ya ARTS.
Tuma barua yako
ya maombi ya
ufadhili wa masomo
kwenda kwa :
MKURUGENZI MTENDAJI,
RAFIKIELIMU
FOUNDATION,
S.L.P 35967,
DAR ES SALAAM.
* Katika barua
yako ambatanisha barua
ya serikali ya
mtaa unaoishi, cheti chako
cha kuzaliwa ama Hati
ya Kiapo " AFFIDAVIT "
, picha zako nne za
rangi, pamoja na vielelezo
vingine vinavyo thibitisha
kwamba wewe ni
yatima.
* Maombi yako yatufikie
kabla ya tarehe
07 JANUARY 2013.
* Maombi yanaweza
kutumwa na msimamizi
wa mwanafunzi husika
kwa niaba yake.
Kwa maelezo zaidi tembelea ; www.
rafikielimu. blogspot.com
No comments:
Post a Comment