Monday, December 17, 2012

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI 192 NA KUFUNGUA MAKTABA YA CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI


Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha, Jumamosi Desemba 15, 2012 tayari kutunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi 192 waliohitimu chuoni hapo.
Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  gwaride la  maafisa wanafunzi katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha.
twendeee.
twende huku nako!
Mwanangu kazi ya jeshi ugangamale!
Gwaride la  maafisa wanafunzi katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha

Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa  maafisa wanafunzi 192  katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha. Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi kamtaba ya kisasa  katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha,
Rais Kikwete akikagua maktaba
Maktaba kwa nje!
Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitembelea bweni namba 15 ambamo Rais Kikwete alikuwa akiishi wakati akiwa mafunzoni hapo  katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha.
Mheshimiwa Rais naomba kukupiga picha msichana Shalom anamwambia Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete   katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha.

No comments:

Post a Comment