Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano hilo.
Hapa ni wakati Nassib, akiingia ukumbini hapo
kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Hapa ni wakati Miyayusho akiingia ukumbini
hapo kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Miyayusho
(kulia) akichapana na Nassib.
Miyayusho (kushoto) akipanga ashambulizi.
Piga nikupige
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo, Dkt. Fenella Mukangara, (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto (wa pili kulia) Ben Kisaka na Mratibu wa pambano hilo, Bawazir, wakiwa
meza kuu wakishuhudia ndonga hizo.
Jamaa sijui analalama nini.
Hapa, Nassib
akijihami kwa kumkumbatia Miyayusho ili kupunguza kasi ya mashambulizi, jambo
ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kumkata pointi kutokana na kukumbatia
kila mara.
Ohooooh!!! Kushney, ''Nasikia Kizungu zungu
kichwa kinaniuma'', Nassib alisikiza akimwambia msimamizi wake, huku
akihesabiwa na mwamuzi wa mchezo huo.
Mashabiki
wakimnyanyua juu Miyayusho, na kushangilia baada ya kutangazwa mshindi katika
pambano hilo.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara,
akimvisha mkanda wa Ubingwa WBF, Francis Miyayusho, baada ya kumtwanga kwa KO,
mpinzani wake Nassib Ramadhan, katika pambano lao la kugombea ubingwa huo
lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Saalaam.
Miyayusho alishinda kwa KO katika rauindi ya 10 kati ya 12 za mchezo huo.
Kushoto ni mratibu wa oambano hilo, Bawazir
Miyayusho akishangilia ushindi huo na
mashabiki wake huku akiwa na mikanda yote miwili aliyokabidhiwa.
No comments:
Post a Comment