Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akizungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba
alipomtembelea ofsini kwake leo. Naibu waziri huyo yupo Mkoani Rukwa ambapo
atatembelea bandari ya Kasanga, Kipili, uwanja wa ndege wa Sumbawanga na eneo
lilitengwa tangu mwaka 1984 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege
katika kijiji cha Kisumba km 20 kutoka Mjini Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akisisitiza jambo
ambapo amemuomba Naibu waziri wa Uchukuzi (Kushoto) kuongeza nguvu katika
kuimarisha miundombinu ya bandari na anga katika Mkoa wa Rukwa ambao unahitaji
sana huduma hizo. Akizungumzia usafiri katika ziwa Tanganyika alisema ziwa hilo
linahudumiwa na meli mbili ikiwemo Meli kongwe kuliko zote duniani inayobeba
abiria ya Mv. Liemba ikiwa na umri wa miaka 100. Meli nyingine ni Mv. Muongozo
ambazo hazikidhi mahitaji ya usafiri kwa wananchi wa mwambao. Alisema pia kuwa
usafiri katika ziwa hilo ni muhimu katika kuimarisha biashara na nchi jirani za
Kongo DR, Burundi na Zambia.
Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed
Chima.
Naibu waziri wa
Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ofsini kwake leo
alipomtembelea ambapo atakuwa Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi. Waziri huyo pia
atafanya ziara katika Mikoa ya Katavi na Kigoma ambapo atakagua miundombinu ya
Reli, Anga, na Bandari. Alimuahidi Mkuu huyo wa Mkoa kuwa Wizara yake
imejipanga kuhakikisha miundombinu hiyo inaimarika Mkoani Rukwa kuwezesha
bidhaa na mazao ambayo huzalishwa kwa wingi Mkoani humo kusafirishwa kirahisi
kwenda katika maeneo yenye masoko.
No comments:
Post a Comment