Tuesday, March 26, 2013

KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5 AU FAINI MIL 13, WEMA AJIANDAA KUMLIPIA


Wema na Kajala akipunga mkono kwa jamaa waliofika mahakamani
Baada ya hukumu, akahojiwa na waandishi habari.


HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Taarifa ni kwamba msanii Wema Sepetu anajiandaa kupeleka faini ya shilingi milioni 13 ili kumnusuru na kifungo msanii mwenzake.
 Tabasamu la Wema laleta matumaini kwa Kajala, nyuma mwenye kilemba cheusi ni Zamaradi Mketema wa movie leo a.k.a  Mama Juju.
 Baba Kajala (kushoto) akishauriana jambo na wasanii wa filamu na maswahiba wa mwanaye

 Hata hivyo baada ya hukumu kutolewa wasanii wa filamu nchini walikuwa wamefika mahakamani hapo kufuatilia hukumu ya kesi hiyo, walikusanyika katika viunga vya mahakama hiyo na kuanza kujadiliana ili wachangishane fedha lakini msanii Wema Sepetu aliwataka wenzake wasichanganishane fedha ,badala yake yeye analipa Sh.milioni 13 na akaondoka katika eneo hilo na kisha kurejea mahakamani hapo saa saba mchana na kulipa faini hiyo na kisha kuondika na Kajala ,wakati Chambo akirudishwa gerezani kwani alishindwa kulipa fidia hiyo na pia anakabiliwa na kesi nyingine ya utakatishaji fedha mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment