Monday, March 25, 2013

MAAFA YA MVUA DAR: MMOJA AMEFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAFURIKO; DARAJA LAFUNIKWA NA MAJI KIMARA


Maji yamezizingira nyumba za bonde la Jangwani, Kinondoni Dar es Salaam.

 Wananchi wametahayari wakitafakari jinsi ya kuvuka ng'ambo ya pili na mustakabali wa daraja hilo.
 Mtaa wa Azikiwe ukiwa umefurika maji 
 
Dar es Salaam -- Habari  zinaeleza  kuwa mvua kubwa iliyoanza kunyesha majira ya saa nne jana  asubuhi imesababisha kifo cha mtu mmoja baada kuzolewa na maji ya mvua hiyo huko Tabata Relini, Ilala.
Blogu ya Josephat Lukaza nayo ina taarifa kuwepo kwa taharuki miongoni mwa wakazi wa Kimara-Kilungure kutokana na daraja la eneo hilo kufunikwa kwa maji ya mvua.

No comments:

Post a Comment