Wednesday, March 20, 2013

MAKALIO KWELI KIBOKO!



Nazungumzia hiyo milima miwili mikubwa!



Nataka ntoe sifa kwa kalio au  makalio! Ningeweza kutamka kama liitwavyo! Ila kutokana na heshima yetu sisi watanzania  natumia tafsida kidogo ili tusikerane, makalio jamani makalio, acheni yaitwe makalio, naomba nikuulize mdau wa hii blog yangu kua usha wahi kuumwa makalio?, ushapata ajali ukaumia makalio? Vyote vyaeza umia lakini sio makalio!

Mwanafunzi darasani hachapwi kichwani,bakora zote zinamalizikia kwenye makalio, hata ukiumwa koo, sindano zote  makalio au kalio, ukichoka! Unakalia makalio, nguo ukivaa unaanzia ama zinashia kwenye  makalio. Makalio ama kalio LINAVULIA hadi harufu mbaya na makapi yanayopita jirani nayo, du! Hebu pumua kidogo uyafariji makalio! Siku njema.


No comments:

Post a Comment