Tuesday, March 26, 2013

WAZIRI WA UCHUKUZI AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA WA TANZANIA NA UJUMBE WAKE OFISINI KWAKE



Waziri wa Serikali ya Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwkyembe(Mwenye suti Nyeusi), wakati alipomtembelea waziri Mwakyembe ofisini kwake mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Balozi wa Uingereza Tanzania, Dianna Melsone.

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye suti nyeusi) akimuonyesha Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds Miradi mbali mbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kwa hapa Tanzania. Waziri Mwakyembe alikutana na Waziri huyo ofisni kwake kujadiliana kuhusu Usafiri wa Anga, Miradi ya Bandari na Miradi mbalimbali ya Reli.

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,akisisitiza jambo kwa  Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(kushoto kwa Waziri Mwakyembe),
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Uingereza  anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(mwenye tai ya blue bahari), Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melsone(kushoto kwa Waziri Mwakyembe) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(Kulia kwa Waziri Mark).

Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akishikana mikono na Waziri wa Uingereza  anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds,

No comments:

Post a Comment