Hii leo wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria
chini ya katiba mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.Taarifa
zinazohusianaKenyaKinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee
wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi
upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.Unaweza kututumia
maoni yako kuhusu uchaguzi kwenye ukurasa wetu wa Bofya facebook
Waziri mkuu Raila
Odinga ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera.
Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa na
hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa shwari
Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa
kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa kupiga kura kunachukua takriban
dakika 12 minutes
Polisi wamepata mwili
mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la
Moshomoroni, mjini Mombasa, Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za
polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa
Mombasa.
mjini Nakuru kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni
ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe , Fatma Sanbur yuko mtaani
Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni.
Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja tangu
waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli yab upigaji kura ilikuwa
haijaanza
William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya
unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani
kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa, UpigaJI kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za
Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma
na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao
Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza
kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa
kuanzia saa tisa usiku tangu kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo
hili hawajawai kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona
foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa
nane usiku. Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa
upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na
vifaa vyao
No comments:
Post a Comment