Mmoja wa wale waliojeruhiwa
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa watu 10,
wakiwemo maafisa wa polisi wawili, wameuawa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya.
Tukio hilo lilitokea alfajiri, kuamkia leo wakenya wanapopiga kura.Hata hivyo
polisi walithibitisha vifo vya maafisa wao wawili vilivyotokea wakati polisi
walipowapiga risasi washambulizi waliokuwa wamejihami kwa mapanga. Lilikuwa
shambulizi la kulipiza kisasi.
Washambulizi hao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani
la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la
Pwani.
Mwandishi wa BBC, Karen Allen, anasema polisi waliweza
kuthibitisha vifo vya wanne katika eneo la Changamwe, naye Hassan Majid aliona
mtu mmoja kauawa eneo la Mishomoroni. Mwtu mwingine Moja ya miili hiyo ilikuwa
imekatwakatwa.
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa miaka mitano iliyopita katika
ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment