Rajo (mbele) akiwa na mwanaye na waume zake watano.
MWANAMKE, Rajo Verma, 21, mkazi wa mjini Dehradun, India, anaishi na wanaume wake watano katika kibanda chenye chumba kimoja ambapo hulala na mwanamme mmoja kila usiku. Mwanamke huyo hana uhakika na baba wa mtoto wake mdogo wa kiume ambapo anasema: “Mwanzoni niliona matatizo kuwahudumia wote katika kuwapa unyumba. Lakini sasa nawahudumia wote bila upendeleo.” Mumewe mmoja aitwaye Guddu, 21, ambaye alikuwa wa kwanza kumwoa anasisitiza: “Wote tunafanya naye tendo la ndoa bila wivu.
Rajo na familia yake wakiwa mbele ya kibanda chao chenye chumba kimoja.
Sisi sote ni familia moja yenye furaha. Jamaa
huyo alimwoa Rajo miaka minne katika ndoa ya mila za Kihindu na ndiye mumewe
halisi. Lakini mila kijijini kwake zilimlazimu kuwachukua kaka za mumewe pia
kama waume zake. Hao ni Bajju, 32, Sant Ram, 28, Gopal, 26, na Dinesh – ambaye
alimwoa kwa njia hiyo ya kimila mwaka jana alipofikisha umri wa miaka 18. Bajju
ambaye ndiye mkubwa kuliko wote anasema: “Namchukulia kama mke wangu na ninalala
naye kama wanavyofanya ndugu zangu.”
Rajo anafanya kazi zote za nyumbani na kumtunza
mtoto wake aitwaye Jay, mwenye umri wa miezi 18, ambapo waume zake huenda
kufanya kazi kila siku mjini Dehradun. Mwanamke huyo anasema mama yake pia
aliwahi kuolewa na ndugu watatu wa kiume, hivyo hilo si jambo la ajabu kwake.
“Ninalala nao kwa zamu. Hatuna vitanda chumbani bali tunatumia mablanketi
yaliyotandikwa sakafuni. Watu hao hunijali na kunipenda zaidi, jambo ambalo
wanawake wengi zaidi hawalipati katika ndoa zao,” anasema.
Chanzo: GLOBAL
PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment