Thursday, March 7, 2013
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA MUSOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, wakifurahia kwa pamoja baada Makamu kuweka Jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Machi 5, 2013 Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Wanachama wa CCM mkoa wa Mara katika Ukumbi wa CCM mkoa uliopo eneo la Nyasho Musoma mjini.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo na kuoneshwa Ramani za ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma, wakati Makamu alipofika eneo hilo kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa nyumba hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBA, mara baada ya Makamu kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Umma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma Mjini Mkoa wa Mara, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mukendo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee wa mkoa wa Mara wakati akiagana nao baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo.
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara.
Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakionyesha umahiri wao wa kupuliza 'midomo ya bata' wakati wa bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment