Monday, March 11, 2013
MWANAMAKUKA AWARD 2013 ILIVYOFANA
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na uksherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2013.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Wanawake Duniani.
Washiriki wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka, wakipita jukwaani wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, ambapo zawadi hizo zilikabidhiwa na Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.Juhaina Kussaga akipita mbele ya wageni.
Mbunifu na mwanamitindo akikjiandaa kuonesha miondoko ya twiga na vazi lake. jina sikulipata niwie radhi mrembo.
Ritha Paulsen wa BSS naye yumooo! huku ni kwa nyuma.
Madam Ritha akiwa amemakinika! mikogo mwake mwake.
Mama Asha Bilal, akishiriki pamoja na wageni waalikwa kuburudika kucheza muziki wa kizazi kipya wa Msanii Q-Chilla, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mwanamakuka zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Mwanamke Duniani.
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini waliofanikisha kufanyika kwa hafla hiyo ya utoaji tuzi za Mwanamakuka 2013, baada ya kukabidhi tuzo hizo kwenye hafla hiyo iliyofanyika machi 8, 2013 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment