Waziri wa uchukuzi amatembelea yalipotunzwa mataruma yaliyoibwa
katika
vipindi tofauti kuanzia mwaka jana mpaka mwezi wa pili mwaka
huu.Magunia
yaliyotumika kufunikia mataruma ya Reli ambayo yaliibiwa na kusafirishwa
kutokea Tabora tarehe 14/2/2012 na kubebwa kwenye Lori la Mizigo la Kampuni ya Unga
ya Azania (linaloonekana mbele) kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza kama
chuma chakavu. Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Dkt. Charles Tizeba wamefanya ziara ya kuangalia mataruma hayo jijini Dar es
Salaam. Mataruma hayo yamehifadhiwa katika yadi ya Reli iliyoko Mivinjeni
Kurasini, Dar es Salaam.
Mataruma ya reli yaliyoibwa!Waziri wa Uchukuzi,
Dkt Harrison Mkwakyembe(mwenye tai nyekundu), akiangalia mataruma 35 yaliyoibiwa
kutoka katika stesheni ya Reli ya Pugu na kusafirishwa kuja Dar es Salaam kwa
ajili ya kuja kuuzwa kama chuma chakavu . Kulia kwa Waziri wa Uchukuzi ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa tai ya mistari).
shehena ya mataruma ya reli iliyokua safarini kwenda kusikojulikana.Shehena ya mataruma ya
zaidi ya Tani 15 yaliyokamatwa na askari wa kikosi cha reli yakiwa katika eneo
la reli Mivinjeni baada ya kukamatwa tarehe 14/2/2013 na dreva wa Lori hilo
kukimbia. Waziri wa Uchukuzi na Naibu Waziri wamefanya Ziara katika eneno hilo
kujionea mzigo wa Mataruma yaliyobiwa katika vipindi tofauti tofauti.
miundo mbinu ya reli ikiwa imekusanywa kwa wingi, je tunaipenda nchi yetu kweli? kwa hali hii hatutafika.Waziri wa
Uchukuzi.Dkt Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu),akipata maelezo kutoka
kwa ACP Saada Haji Mkuu wa kikosi cha Polisi (Reli)(aliyevaa hijabu) ya namna
wezi wa Mataruma hayo walivyoiba na kukamatwa na askari wake tarehe 14 Februari
2013. Kulia kwa ACP Saada Haji, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt
Charles Tizeba.
I see kazi nzuri kwa mliokamata miundo mbinu ya reli! juhudi zifanyike za kuwakamata wahujumu hao wa mali ua umma!Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akipata maelezo na mataruma yaliyobiwa kutoka kwa
ACP Saada Haji ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi Cha Polisi Reli, wakati walifanya
ziara ya kuangalia mataruma ya reli yalyibiwa katika vipindi tofauti tofauti
yaliyopo katika eneo la Mivinjeni kurasini
No comments:
Post a Comment