Tuesday, March 19, 2013

ZIARA YA KAMATI YA MIUNDOMBINU



Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti nyeusi), akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Miundombinu wa namna usafiri wa treni Dar es Salaam unavyofanya kazi, katika kituo cha Stesheni ya Dar es Salaam jana  asubuhi . Kamati ya Miundombinu imetembelea usafiri wa treni ya Dar es Salaam ya Shirika la Reli Tanzania (TRL
) kujionea namna usafiri huo unavyofanya kazi.


Wabunge wa kamati ya Miundombinu wakiwa katika mojawapo ya mabehewa yanayofanya safari zake kutokea stesheni ya Dar es Salaam mpaka Ubungo. Kamati ya Miundombinu imetembelea usafiri huo na kujionea namna unavyofanya kazi, ambapo walipanda treni hiyo kutokea Stesheni ya Dar es Salaam mpaka Ubungo na kurudi.

Mhandisi Richard Lauwo, akitoa ufafanuzi wa  sehemu za kupandia treni(Platform) zilivyojengwa na Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli( RAHCO) kwa Mwenyekiti ya Kamati ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba(Mb), katika stesheni ya Ubungo Maziwa.
 
Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba (Mb) akishuka kwenye Stesheni ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara iliyoifanya na wajumbe wa  kamati hiyo

No comments:

Post a Comment