Mwili wa aliyekua WP2492 Koplo Elikiza Nnko ukifunikwa eneo la tukio.
aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari.
MTANDAO wa GPL jana mchana umeripoti taarifa ya ajali ya Askari wa
Usalama wa Barabarani, WP2492 Koplo Elikiza Nnko, aliyegongwa na gari eneo la
mataa ya Bamaga. Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kinondoni, Charles Kenyela, ni kwamba amefariki dunia.
Akizungumza na Wapo Radio FM kwa njia ya simu akiwa katika
hospitali ya Taifa Muhimbili, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles
Kenyela alisema marehemu WP2492 Koplo Elikiza Nnko wa Usalama wa Barabarani,
baada ya kupewa taarifa kuwa magari ya msafara wa Rais yameshapita yote,
alirudi barabarani ili kuongoza magari mengine pasipo kujua kuwa kuna gari
linakuja kwa kasi. Dereva mwenye gari aina ya Landrover Discovery lenye namba
za usajili T328BML mali ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), alipoona
msafara… huo, umepita aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla
gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.
(Picha na Shauri Kati / GPL)
No comments:
Post a Comment