Papa Benedict amefanya misa yake ya mwisho hadharani kabla
ya kujiuzulu rasmi hapo kesho, kitendo kama hicho kilifanyika katika Kanisa
Katoliki miaka mia sita ilyopita.
Amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika viwanja vya
Mtakatifu Petro huko Vatican kwamba alikuwa anafahamu uzito wa aamuzi wake
lakini amefarijika kutokana na imani yake kwa Mungu na Kanisa Katoliki.