Saturday, June 30, 2012

Lauryn Hill & Wyclef - Killing me softly

                                          



wimbo ndo huu ulompa umaarufu Luryn Hill, endeleaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!

Lauryn Hill Huenda akakabiliwa na Miaka Mitatu jela


                                                Lauryn Hill

Kama utakumbuka niliwahi kuandika humu bloguni kuhusiana na kesi inayomkabili mwanamuziki magiri,mzuri na mwenye ngozi mwanana Lauryn Hill kwa kutolipa kodi.
Hivyo basi, Kwenye Mahakama moja ya New Jersey , kesi ya Lauryn Hill iliendelea kusikilizwa  ambapo staa huyu wa muziki yuko kwenye hatari ya kwenda jela kwa miaka mitatu kutokana na kukwepa kulipa kodi ya dola za kimarekani milioni 1.8 kati ya 2005 and 2007, ambapo atatakiwa kuanza kutumikia kifungo chake November mwaka huu.
Kwa muujibu wa  AP Staa huyo amekutwa na hatia baada ya kukiri kwamba alishindwa kulipa kodi kwa sababu za kuikimu familia yake,  kitu ambacho ni kosa la kisheria
mmsanii huyo aliyetwaa tuzo za grammy mara 8,mwenye miaka 37 ,alikhukumiwa mwezi huu kwa kushindwa kulipa kodi ya Internal Revenue Service miaka kadhaa.Na alipotakiwa kukubali kosa ama kukataa, Hill alikubali kosa kwa kusema ndio sijalipa kodi kwa miaka hiyo yote.
Kwa muujibu wa wakili wa mwanamuziki huyo Nathan Hochman, Hill  amekubali kulipa kodi anayodaiwa  . Hill alikubali kua hajalipa kodi kwa mapato yake kama dola za kimarekani 818,000 alizopata mwaka  2005, dola 222,000 alizopata mwaka 2006 na dola  761,000 alizopata mwaka  2007.
Mbali na kukubali kulipa kodi anayodaiwa atapigwa fine ya dola 75,000 .Hill aliachiliwa kwa gharama ya dola 150,000  , na hukumu ya kifungo chake itasikilizwa November mwaka huu.

Friday, June 29, 2012

Kesi ya Rihanna Kupigwa Na Chris


                                       Rihanna

Polisi wawili wa jiji la Los Angeles hawatakabiliwa na makosa ya jinai kwa kuhusika kuachilia picha ya nyota wa pop Rihanna akiwa na madonda aliyoyapata kwa kupigwa na aliyekua mpenzi wake Chris Brown mahakama ya jiji hilo la Los Angeles imetoa tamko hilo
Na hii ni baada ya uchunguzi uliochukua miaka 3 ,wachunguzi wamedai kua hawana ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani maofisa hao.

Maofisa hao ni Blanca Lopez na Rebecca Reyes pamoja na kuepuka kuingiza hatiani, bado hawako salama, watatimuliwa kazi kwa kukosa nidhamu kazini.na kutakua na kikao cha kinidhamu mnamo mwezi August.

                                      Rebecca Reyes

                                        Blanka Lopez

                                            Chris na Rihanna

Brown, ambaye alikua ni mpenzi wa  Rihanna's  wakati huo alikamatwa kwa kumpiga mshindi huyo wa tuzo za Grammy winner mwezi Feb.tarehe  8,  mwaka 2009, na kumuachia majeraha na mvio wa damu.
Na hivyo kusababisha aahirishe kufanya show kwenye tuzo za Grammy mwaka huo kufuatia ajali hiyo.
Brown alikutwa na hatia ya kumshambulia Rihanna aliamuriwa kwa miaka mitano kua chini ya uangalizi na kutimiza miezi 6 ya huduma za jamii,ikiwemo usafi wa barabra na mengineyo
Reyes na Lopez walikua wanakaa chumba kimoja wakati huo walimpiga picha Rihanna na kuzitupia kwa watu wa Fox Television na TMZ mnamo mwezi February.

                                          Picha Za TMZ

Picha ambazo ziliwashtua mashabiki wa Rihanna na Brown na kuzusha mjadala mzito kabla hata hazijatua katika vyombo vingine vya habari. Na walilipwa mijihela ila walipofuatiliwa katika accounts zao bank hawakukutwa na kitu
 Katika kutaka kuwaonesha askari hao wathibitishe kua hawakuhusika kuachilia picha za Robyn F. (Rihanna) kwa  TMZ  kwa mabadilishano na pesa laikini pia wanakabiliwa na shutuma za kushadidia uhalifu kwa kusambaza picha hizo.
Wakili wa Rihanna aitwae Donald Etra jana alisema kua hajui kama mteja wake atahitaji kwenda mbele kisheria zaidi ama lah!


UNESCO yahofia usalama wa maeneo ya kale



                                                    Mji wa Timbuktu

Umoja wa Mataifa umeelezea wasi wasi dhidi ya usalama wa mji wa kale wa Timbuktu kaskazini mwa Mali huku machafuko yakiendelea eneo hilo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni{UNESCO} limesema Timbuktu na kaburi la Askia ambalo limekuwepo tangu karne ya 17 katika mji wa Gao ni maeneo yanayokumbwa na hatari. Makundi ya Kiisilamu yameuteka mji wa Gao kutoka kwa waasi wa Tuareg.
UNESCO imeelezea hofu ya tisho la kuporwa kwa baadhi ya kumbukumbu za kale ambazo zimehifadhiwa maeneo hayo.Serikali ya Mali imetaka Umoja wa Mataifa kutambua tisho la usalama wa maeneo ya kale na kusema huenda kukawa na biashara ya magendo ya vifaa vya kale.
Mji wa Timbuktu ambao uko kwenye Jangwa la Sahara una maeneo mengi ya kale ambayo yamedumu kwa karne nyingi licha ya kujengwa kwa udongo na mbao. Mji huo pia umehifadhi nyaraka za kale laki saba kwenye maktaba 60.
Waasi wa Tuareg na wapiganaji wa Kiisilamu wameweza kuyadhibiti maeneo ya Kaskazini mwa Mali baada ya kutokea mapinduzi wa kijeshi nchini humo.
Wadadisi wamesema makundi hayo yana misimamo tofauti ambapo Tuareg wanakata kujitenga huku kundi la Kiislamu likitaka kuwepo Sharia ya Kiisilamu kote nchini Mali.
Kaburi la Askia, lilijengwa mwaka 1495 kwa umbo la Piramidi ambapo amezikwa Mfalme Mohammad Askia, aliyeongoza Milki ya Songhai, ambayo imetajwa kua bora zaidi katika historia ya Milki za Kiisilamu.

Beckham hatashiriki Olimpiki







Aliyekuwa nahodha wa Uingereza, David Beckham, amekosa nafasi katika timu itakayowakilisha Uingereza wakati wa michezo ya olimpiki.
Beckham amesema hakuchaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji katika timu hiyo inayojumuisha wachezaji kumi na wanane.
Amesema kuwa angependa kuiwakilisha Uingereza na amevunjika moyo kutoka na uamuzi huo.

Wakati huo huo!Imebadilishwa: 
Polisi nchini Kenya wamemchukulia hatua mwanariadha mashuhuri Ezekiel Kemboi kwa madai ya kumdunga kisu mwanamke mmoja Jumatano usiku.
Kemboi anasifika kwa mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji. Mwanamke anayedai kufanyiwa kitendo hicho, Anne Njeri Otieno ambaye ni mfanya biashara, anadai kuwa mwanariadha huyo alimshambulia wakati alipokataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.


Kemboi, aliambia polisi kuwa wakati alipokuwa anamrejesgha nyumbani mwanamke huyo katika mji wa Eldoret, walishambuliwa na watu wlaiokuwa wamejihami na hivyo akajeruhiwa kwenye purukushani hilo.
Kemboi mwenyewe ni afisaa wa polisi na anajiandaa kwenda mjini London kwa michezo ya Olimpiki.
Hata hivyo Kemboi aliachiliwa kwa dhamana baada ya kulipa dola 595 za Kimarekani na kesi yake itasikilizwa tena mwezi Septemba baada ya michezo ya Olimpiki.
"Tayari niko katika kikosi cha wanariadha watakaowakilisha Kenya kwenye michezo ya Olimpiki. Ninaomba mahakama kunipa nafasi niweze kushiriki " alinukuliwa akisema Kemboi mbele ya mahakama.
Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama Chebusiri anasema kuwa Kemboi alichukua muda wa saa saba katika kituo cha polisi alipokuwa anahojiwa.



Kituo hicho cha polisi pia kilijaa watu waliokuwa wanataka kumuona Kemboi alipofika kwa mashtaka.
Hapo awali, Bi Otieno, ambaye anaendelea kupata nafuu hospitalini, aliambia waandishi wa habari kwamba alikuwa kwenye mkahawa mmoja na Kemboi wakati alipokubali kumpeleka nyumbani usiku ulipoingia.
Mwaka 2004 Kemboi aliyeshinda dhahabu kwenye mbio za elfu tatu aliambia polisi kuwa alivamiwa na wezi alipokuwa nje ya gari lake na kumtaka awape pesa na kisha kumshambulia.
Alisema alichukua hatua hiyo ili kujilinda dhidi ya kuvamiwa na katika purukushani hiyo Bi Otieno akajeruhiwa

Thursday, June 28, 2012

Wanaijeria Watakiwa Kupanga Uzazi


                                           Rais Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anasema wakati umefika raia wake kupanga uzazi. Kiongozi huyo amesema kuna watoto wengi sana wanaozaliwa na ipo haja kuwepo na sheria ya kuwa na mpango wa uzazi.
Ameongeza watu wasio jua kusoma wala kuandika wameendelea kuwapata watoto wengi ambao wanashindwa kuwapa mahitaji muhimu ya maisha.Umoja wa Mataifa unakadiria idadi ya Nigeria kuongezeka kutoka milioni 160 hadi milioni 400 ifikapo mwaka 2050.
Nigeria inaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya watu Afrika na juhudi za awali kuwashawishi wazazi kuwapata watoto wachache ziligonga mwamba.Mwandishi wa BBC Will Ross amesema ongezeko la watu linapunguza raslimali hali inayotishia kuwepo na machafuko ya kushindania raslimali hususan ardhi.
Rais Jonathan amesema ipo haja kuwepo na sheria ya kudhibiti idadi ya watoto wazazi wanaopata katika siku za usoni.Amelitaka Baraza la Idadi ya watu kuanza kampeini ya kushawishi jamii umuhimu wa mpango wa uzazi.


                                                            kina mama sokoni

Amesema japo suala hili ni nzito kutokana na misimamo ya kidini na kimila, ipo haja jamii kubadilisha mawazo kwamba watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.


Wednesday, June 27, 2012

Amitha Batchan ahofiwa Kufa



Inasemekana kua Amitabh Bachan  amefariki katika ajali ya gari kati ya Morristown na  Roswell. Shuhuda wa ajali hiyo alieleza kua alitambua kua mtu aliyepata ajali ya gari ni Amitha kwa kuona kitambulisho kilichokutwa kwenye mwili wake.
Taarifa zinaeleza kua chanzo cha ajali hiyo si dawa za kulevya wala pombe.
Wachunguzi wa Highway Safety Investigators  wanaeleza kua Amitabh Bachan alipoteza muelekeo na gari alilopata nalo ajali ni la rafikiye na gari hiyo ilibinjuka mara kadhaa wakati ajali hiyo ilipotokea na kudaiwa kua alikufa papo hapo.
 inakadiriwa kua gari hiyo ilikua kwenye mwendo wa speed 95  kwa saa

tusubiri taarifa zaidi ,maana hii ni shaka shaka tu kwa muujibu wa GLOBAL ASSOCIATES NEWS.


                                          Gari alopata nalo ajali Amitabh Bachan

Askofu Afumwa Akila Bata, Picha zarushwa live Runingani






Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa 16 ameikubali barua ya kujiuzulu ya Askofu wa Argentina na hiyo inafuatia baada ya picha ya Askofu huyo kuoneshwa hadharani hivi karibuni akiwa katika moja ya fukwe za mexico akiwa amekumbatiana kimapenzi na mwanamke aliyekua amevalia bikini

 

Askofu huyo aitwae FERNANDO BARGALLO, alipigwa picha hizo zikimuonesha akiwa amezama kibahaba na mwanamke aliyekua amevaa nguo za kuogelea zenye kuanika maungo yake yote yanayoonekana kumpagawisha Askofu FERNANDO

 
Askofu FERNANDO BARGALLO, alikua akihudumu katika jimbo la MERLO MORENO katika jiji la BUENOS AIRES na kashfa hiyo ilirushwa live na kituo cha television cha taifa hilo na kuonesha picha chafu za Askofu huyo akijivinjari wakati alipokua kwenye mapumziko katika fukwe tulivuuuuuuuu!

 
Kufuatia kashfa hiyo , tayari makao makuu ya kanisa katoliki huko VATICAN imemteua MONSIGNOR ALCIDES JORGE PEDRO CASARETTO, kuchukua nafasi ya askofu huyo aliyejiuzulu kwa hiari yake ili aendelee kula bata ,kwa uwazi na nafasi na mrembo wake.

Tuesday, June 26, 2012

Mbwa dili China






Kila taifa lina utamaduni wake na vyakula vya asili vya makabila yaliyomo katika taifa hilo.lakini vyakula vingine vinastaajabisha kiasi cha ile methali ya Tanzania kupata mashiko zaidi, UKISTAAJABU YA MUSA! UTAONA YA FIRAUNI!!
Nimeileta kwa sababu, huko china nyama maarufu iliwayo sio ya ng’ombe,mbuzi na wengineo lah hasha bali mbwa,paka,mamba na wengineo wamekua kitoweo maarufu kuliko kawaida, hivyo nitumie fursa hii kuwatahadharisha watanzania wenzangu waendao China ambao pengine wana uchu wa nyama wakiwa nyumbani, wajizuie kidogo katika nchi za watu wanaweza kulishwa mifugo hiyo!


         mbwa hao wameshanunuliwa tayari kwa biashara.!!!! 

Kikundi cha Wanaharakati wa mjini Yulin, katika jimbo la Guangxi,  wamelipinga soko la biashara ya nyama ya mbwa na kuwaomba watu wa eneo hilo kutokula nyama ya wanyama hao.


  wanapelekwa buchani tayari kwa kuuawa,kuchinjwa  ama   kupelekwa katika soko la  nyama la Guangxi.


Wachina walio wengi wana enjoy sana  kula nyama ya mbwa, hasa kipindi cha majira ya  baridi na miji mingine huwapiga mbwa hadi kifo ili kuruhusu damu ya mbwa itoke katika nyama.


Mpishi akikaangiza nyama ya mbwa , ona mwenye uchu unaweza kuingia mkenge! anaandaa mlo wa jioni.


tabasamu tele usoni dada huyu na familia yake wakipata mlo wa jioni , kitoweo nyama ya mbwa.utamaduni huu ni wa miaka mingi iliyopita.


               sehemu ya machinjio,uchunaji na uandaaji wa nyama ya ng'ombe.

Wakati kukiwa na uhaba wa chakula, basi mbadala wa chakula ni nyama ya mbwa kama chakula cha dharura maeneo mengi ya China utaratibu ama zoezi ambalo limekubalika na Wachina walio wengi.
Mnamo mwezi April, zaidi ya mbwa  500  walikua wameandaliwa kwa kuuawa ,gari iliyokua imewabeba kuwapeleka katika nyumba ya kuwachinjia  ilipo zuiliwa na wanaharakati za wanyama.
Mbwa  505 waliokoka katika hatari hiyo na hali za kuwadhuru na mbaya zaidi huwa hawanywi maji wakati wa safari yenye urefu wa 1,000  kwa bara bara,ingawa mbwa 11 waliishiwa maji mwilini na walikutwa na hali mbaya .


watu wakijisevia mgahawani ,kama uonavyo jibakuli liko kati jichotee tani yako.

  
                         mtaani anauzwa mbwa kama kawaida 

unaweza kula nyama ya mbwa kwa tambi na mazaga zaga mengi tu! familia ikiendelea.