AU inasema kuwa Rais
Kenyatta atakosa mikutano muhimu kwa sababu naibu wake atakuwa Hague.
Muungano wa Afrika sasa
unataka mahakama ya kimataifa ya ICC kusitisha kesi za Naibu rais wa Kenya
William Ruto, Rais Uhuru Kenyatta na mwandishi Joshua Arap Sang katika mahakama
hiyo hadi pale ombi lake kwa mahakama hiyo kutaka kesi hizo kurejeshwa nyumbani
kuamuliwa.
AU pia inataka Bwana
Ruto na Rais Kenyatta kuruhusiwa kuchagua vikao wanavyotaka kuhudhuria wakati
wa kusikizwa kwa kesi zao kutokana na majukumu yao ya kikatiba.
Kwenye barua
iliyoandikwa kwa ICC, AU inasema kuwa mahakama hiyo mwanzo ilipaswa kuamua
ikiwa itaweza kuhamishia kesi hizo nchini Kenya kabla ya hata kuanza
kuzisikiliza.
Katika barua yake kwa
ICC, AU pia Imegusia swala la rufaa ambayo imewasilishwa katika mahakama hiyo
na mwendesha mkuu wa mashtaka Fatou Bensouda dhidi ya kumruhusu bwana Ruto
kuhudhuria tu baadhi ya vikao akisema kuwa majaji wangemlazimisha naibu rais
Ruto kuhudhuria vikao vyote vya kesi yake kabla ya rufaa kuamuliwa.
Muungano huo umeelezea
kuhusu mikutano mikuu miwili ya usalama inayotarajiwa kufanyika baadaye mwezi
huu ambayo Rais Kenyatta hataweza kuhudhuria kwa sababu kesi ya naibu rais
William Ruto itakuwa inasikilizwa ICC.
AU imeongeza kuwa kesi
hizo zitahujumu jukumu la Kenya katika ukumbi wa kimataifa ikisisitiza kuwa
hazipaswi kuathiri majukumu ya viongozi hao wawili.
AU inasema kuwa licha
ya kuwa Kenya imekuwa ikiheshimu mahakama hiyo, inapaswa kufanya hivyo kwa
kuzingatia Katiba yake.
No comments:
Post a Comment