Tuesday, September 17, 2013

RWANDA YAFANYA UCHAGUZI WA BUNGE KWA UTULIVU

 


Wanyarwanda milioni 6 kati ya watu milioni 11 nchini Rwanda jana ambayo ilikuwa siku ya taifa ya Rwanda walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa bunge la nchi hiyo. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa mchana.

Huo ulikuwa ni uchaguzi wa tatu wa bunge kufanyika nchini Rwanda tangu nchi hiyo ikumbwe na mauaji ya halaiki. Wagombea kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa na wagombea huru wanagombea nafasi 53 za viti 80 vya ubunge. Viti 27 vilivyobaki vimetengwa kwa ajili ya wajumbe wa viti maalum ikiwa ni pamoja na vya wanawake, vijana na walemavu.

Kabla ya uchaguzi chama tawala cha Rwanda RPF kilikuwa na viti 42 kati ya viti 53, na muungano wa vyama vingine vinne kila kimoja kikiwa na viti viwili.

No comments:

Post a Comment